Snow White and the Seven Dwarfs (filamu ya 1937)
Snow White and the Seven Dwarfs (kwa Kiswahili: Mweupe Theluji na Vibete Saba) ni filamu ya katuni ya mwaka wa 1937 kutoka Marekani iliyotokana na ngano za kale ya akina Grimm, Mweupe Theluji. Ilikuwa filamu ya kwanza kuwa na kipengele kirefu katika historia ya filamu za katuni, vilevile kuwa kama filamu ya kwanza ya katuni kutayarishwa nchini Marekani, ya kwanza kutayarishwa kuwa na rangi kamili, yaani, mwanzo hadi mwisho, ya kwanza kutayarishwa na Walt Disney, na ni ya kwanza katika mfululizo wa filamu za katuni za Disney - Walt Disney Animated Classics.[2]
Snow White and the Seven Dwarfs | |
---|---|
Posta ya filamu | |
Imeongozwa na | David Hand (usimamizi) William Cottrell Wilfred Jackson Larry Morey Perce Pearce Ben Sharpsteen |
Imetayarishwa na | Walt Disney |
Imetungwa na | Brothers Grimm (ngano za kale) Ted Sears Richard Creedon Otto Englander Dick Rickard Earl Hurd Merrill De Maris Dorothy Ann Blank Webb Smith |
Nyota | Adriana Caselotti Lucille La Verne Pinto Colvig Roy Atwell |
Muziki na | Frank Churchill Paul Smith Leigh Harline |
Imesambazwa na | RKO Radio Pictures |
Imetolewa tar. | 21 Desemba 1937 (onyesho la kwanza) 4 Februari 1938 (US) 5 Aprili 1938 (Canada) |
Ina muda wa dk. | Dk. 83 |
Nchi | Marekani |
Lugha | Kiingereza |
Bajeti ya filamu | $1,488,423 |
Mapato yote ya filamu | $8,000,000 (est.) [1] |
Snow White ya Walt Disney ilianza kuonyeshwa kwa mara ya kwanza katika ukumbi wa Carthay Circle Theatre mnamo tarehe 21 Desemba 1937, na filamu ilitolewa katika makumbi mengine na RKO Radio Pictures mnamo tar. 4 Februari 1938. Hadithi hii imechezwa na Dorothy Ann Blank, Richard Creedon, Merrill De Maris, Otto Englander, Earl Hurd, Dick Rickard, Ted Sears na Webb Smith kutoka katika ngano za kale za Kijerumani Snow White ya Brothers Grimm. David Hand alikuwa mwongoza na msimamizi wa kazi hii, wakati William Cottrell, Wilfred Jackson, Larry Morey, Perce Pearce, na Ben Sharpsteen waliongoza vipengele kimoja baada ya kingine cha filamu.
Marejeo
hariri- ↑ Maltin, Leonard (1980, rev. 1987). Of Mice and Magic: A History of American Animated Cartoons. New York: Plume. ISBN 0-452-25993-2.
{{cite book}}
: Check date values in:|year=
(help). Pg. 57 - ↑ Smith, Dave. Disney A to Z, Third Edition, (2006), page 33.
Viungo vya nje
hariri- Snow White and the Seven Dwarfs at the Internet Movie Database
- (Kiingereza) Snow White and the Seven Dwarfs katika Allmovie
- Snow White and the Seven Dwarfs katika Sanduku la Ofisi la Mojo
- Snow White and the Seven Dwarfs katika Rotten Tomatoes
Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Snow White and the Seven Dwarfs (filamu ya 1937) kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |