Mnyanya
(Solanum lycopersicum)
Minyanya
Minyanya
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Asterids (Mimea kama alizeti)
Oda: Solanales (Mimea kama mnavu)
Familia: Solanaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mnavu)
Jenasi: Solanum
L.
Spishi: S. lycopersicum
L.

Mnyanya (Solanum lycopersicum) ni mmea wa familia Solanaceae, ambao daima hutambaa na ambao hukuzwa kwa makusudi ya kutumiwa na watu. Matunda yake yanaitwa nyanya. Kwa aina nyingi sana nyanya huwa na rangi nyekundu pindi inapoiva, nyingine zina rangi ya manjano au machungwa. Mnyanya huwa na urefu wa mita 1-3 na huwa na shina laini ambalo mara nyingi hujibebelesha kwenye mmea mwingine. Majani huwa na urefu wa sentimeta 1-25, na petali 5-9 Majani ya shina la nyanya huwa na vinyweleo. Maua huwa na upana was m 1-2, rangi ya manjano na majani matano na huvunwa kwa mwaka mmoja.

Historia

hariri

Asili ya mnyanya ni Amerika ya Kusini. Na historia huonesha kuwa mimea hii ilianzia huko Peru. Mimea hiyo ya mwanzo ndiyo imekuja kuwa na aina hizi tulizonazo leo za nyanya. Spishi moja ilisafishwa mpaka Meksiko kwa ajili ya matumizi ya binadamu. Ushahidi unaonyesha kuwa hapo awali ulikuwa tunda dogo lenye rangi ya njano.

Neno la Kiingereza ‘tomato’, lenye maana ya nyanya, limetoka ana Nsha ya Manati ‘lomatl’. Mtaalamu wa mmea wa kifaransa, Joseph Pitton de Tournefort, alitoa jina la kisayansi ’Lycopersion esculum’ kwa nyanya, na wakati huo nyanya ilifikiriwa kuwa ina sumu ndiyo maana ilipewa jina la mito lenye maana ya tunda la mbwa mwitu. Watu wa Acret na wengine wanaanza kutumia nyanya kwenye mapishi yao, wakti huo ikilimwa huko Peru, mnamo mwaka 500KK. Baadaye nyanya zilizobadilika na kuwa laini, kubwa kutoka kwenye mboga laini, na kuanza kushamiri huko Amerika ya Mwanzo. Huaminika hii ndiyo asili ya nyanya tunazotumia sasa.

Kulingana na Andrew Smith, aliyeandika kitabu cha ‘The Tomato in America’, nyanya zilianza sehemu za miinuko ya magharibi ya kusini mwa Amerika. Hata hivyo anasema hakuna ushahidi wa kuonesha kuwa nyanya zilikuwepo na hata kuliwa huko Peru kabla ya Wahispania hawajavamia. Nyanya huko Hispania, baada ya utawala wa wahispania huko Amerika, wahispania walisambaza nyanya kwenye makoloni yake yote mpaka Kusini mwa Asia na baadaye Asia yote. Wahispania walipeleka nyanya Ulaya pia. Nyanya zilikuwa nzuri sana huko Mbarka wa Mediteranean na kilimo chake kilianza rasmi mnamo 1540. Nyanya zilianza kuliwa rasmi na huko Hispania mnamo 1600. Mwaka 1692, kilipatikana kitabu kinachoaminika kuwa kilichapishwa huko Naples, kilichokuwa kikielezea mapishi yaliyohusika nyanya kama kiungo.

Uingereza

hariri

Nyanya zilikuwa hazizalishwi huko Uingereza mpaka 1590, kulingana na Smith. Miongoni kati ya wakulima wa mwanzo alikuwa ni John Geral, daktari-Kinyozi. Kitotou Geralds’s Iteneal’, kilichochapishwa mapema 1597, kilizua mjadala wa kwanza kuhusu nyanya huko uingereza. Gereld alijua kuwa nyanya zinaliwa huko Hispania na Italia. Lakini aliamini majani yake yana sumu na tunda lake (nyanya) ni salama. Na hadi kufikia miaka ya 1200, watu wengi walikuwa tayari wanakula sana nyanya.

Afrika ya Kati

hariri

Nyanya ziliingia katika kilimo cha Mashariki ya kati kupitia John Barker, mnamo 1799-1825. Mnamo karni ya 19, matumizi yake makubwa yalikuwa bado ni kama kiungo, na ndio iliyokuwa pekee ikitumika katika maeneo yale. Nyanya ziliingia Mashariki ya kati kutumia njia mbili. Njia ya kwanza ni kupitia uturuki na Armenia na njia ya pili ni kupitia familia ya Mfalme wa Qajar, iliyokuwa mara kadhaa ikisafiri kuelekea ufaransa.

Amerika

hariri

Utambuzi wa kwanza wa nyanya huko Amerika uliripotiwa na William Salmon, mnamo 1710, aliyesoma nyanya zilikuwa huko ambako leo kunajulikana kama South Carolina, Inawezekana zikawa zimeletwa kutoka Karibea, na mpaka sasa watu kadhaa kuona nyanya kama kuwa zina sumu, na ni hatari kula, na hutumika sana kama mmea na mapamo zaidi.