Somagedi ni kata ya Wilaya ya Kishapu katika Mkoa wa Shinyanga, Tanzania.

Somagedi ni kata yenye vijiji vinne ambavyo ni Kisesa, Wimate, Jigulu na Malwilo.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 8,128 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,428 waishio humo.[2]

Katika kilimo wakazi wa Somagedi wanajishugulisha na hasa pamba, mtama, choroko, mpunga (hasa Malwilo), mahindi, alizeti n.k.

Pia wanajihusisha na ufugaji wa ng'ombe, punda, kondoo, mbuzi, mbwa, kuku, bata na mifugo mingine.

Kata ya Somagedi kuna vyama vya msingi vitatu ambavyo vinahudumia wakulima wake hasa wanaolima mazao ya biashara; vyama hivyo ni Imalabupina AMCOS (Kisesa), Wimate AMCOS (Wimate) na Malwilo AMCOS (Jigulu na Malwilo)

Marejeo hariri

  Kata za Wilaya ya Kishapu - Mkoa wa Shinyanga - Tanzania  

Bubiki | Bunambiyu | Bupigi | Busangwa | Idukilo | Igaga | Itilima | Kiloleli | Kishapu | Lagana | Maganzo | Masanga | Mondo | Mwadui Lohumbo | Mwakipoya | Mwamalasa | Mwamashele | Mwasubi | Mwataga | Mwaweja | Ndoleleji | Ngofila | Seke-Bugoro | Shagihilu | Somagedi | Songwa | Talaga | Uchunga | Ukenyenge


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Shinyanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Somagedi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.