Mto Songhua
(Elekezwa kutoka Songhua River)
Mto Songhua (kwa Kirusi: Сунгари, Sungari) ni kati ya mito mikubwa nchini China, pia ni tawimto kubwa la Amur. Songhua ina njia ya km 1,927 kutoka Milima ya Changbai iliyopo kwenye mpaka wa China na Korea Kaskazini kupitia mikoa wa kaskazini ya China.
Chanzo | Milima ya Changbai |
Mdomo | Mto Amur |
Urefu | km 1927 |
Kimo cha chanzo | m |
Mkondo | m3 |
Eneo la beseni | km2 557,180 |
Miji mikubwa kando lake | Harbin, Jilin, Songyuan, Jiamusi |
Mto huo una beseni la km2 557,180[1] [2] ukibeba m³ 2,463 za maji kila sekunde.[3]
Songhua inapita katika tambarare ya China kaskazini iliyo na mtelemko mdogo sana na hivyo njia ya mto ni ya kupindapinda ukiacha mahali penye maziwa madogo kama mabaki ya njia zake za awali.
Marejeo
hariri- ↑ ), National Geographic Society (U.S (2008). National Geographic Atlas of China, p. 36. ISBN 9781426201363.
{{cite book}}
:|last=
has numeric name (help) - ↑ [http://web.archive.org/20190907213106/http://www.riversnetwork.org/rbo/index.php/river-blogs/north-asia/item/4614-amur-river-basin-watersheds-map Ilihifadhiwa 7 Septemba 2019 kwenye Wayback Machine. Amur river basin at Rivers Network
- ↑ National Conditions: Main Rivers accessed October 21, 2010.
Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mto Songhua kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |