Florida ni jimbo la Marekani la kujitawala katika kusini mashariki ya nchi. Umbo lake ni rasi inayoanza Marekani bara kuelekea Kuba. Upande wa magharibi ni maji ya ghuba ya Meksiko na upande wa mashariki maji ya Atlantiki. Upana wa rasi ni kati ya 160 hadi 200 km; upande wa kaskazini kabisa eneo la jimbo lapanuka kama kanda mwambaono wa ghuba ya Meksiko.

Florida

Bendera

Nembo
Nchi Bendera ya Marekani Marekani
Mji mkuu Tallahassee
Eneo
 - Jumla 170,304 km²
 - Kavu 139,670 km² 
 - Maji 30,634 km² 
Tovuti:  http://www.myflorida.com/

Florida imepakana na majimbo ya Marekani ya Georgia na Alabama. Nchi za Karibi za Kuba na Bahamas ni karibu.

Jina la Florida ni ya Kihispania, maana yake ni "yenye maua".

Ramani ya Florida

Jiografia hariri

Florida ina eneo la 137,374 km², ni nafasi ya 22 kati ya majimbo ya Marekani. Upande wa kusini wa rasi kuna kundi la visiwa la "Florida Keys" lenye umbo kama pinde vinavyounganishwa kwa madaraja. Kisiwa cha kusini kabisa ni "Key West" ambayo kipo kwa umbali wa 140 km pekee na Kuba.

Hakuna milima, na mahali pa juu kabisa pana kimo cha 105 m juu ya UB.

Mji mkuu wa jimbo ni Tallahassee, na Jacksonville ni mji mkubwa jimboni. Miji mingine mikubwa ni Tampa, Orlando na Miami. Orlando kuna maonyesho mashuhuri wa Disney Land. Florida ni pia mahali ambako makombora na vyombo vya angani vya Marekani hurushwa kwenye uwanja wa Cape Canaveral unaoitwa pia "Kituo cha Angani cha Kennedy".

Wakazi hariri

Florida ni kati ya majimbo ya Marekani yenye wakazi wasio wachache ambao hawatumii Kiingereza kama lugha ya nyumbani; takriban 16% husema Kihispania.

Kuna wazee wengi kwa sababu ya hali ya hewa pasipo na baridi. Wazee wengi kutoka majimbo ya kaskazini wamependa kuhamia Florida ama kwa uzeeni au kununua makazi wanapokaa wakati wa baridi.

 
Kurushwa kwa chombo cha angani kwenye kiwanja cha Cape Canaveral

Historia hariri

Florida ilikaliwa na Waindio kabla ya kuja kwa Wazungu. Tarehe 2 Aprili 1513 Mhispania wa kwanza alifika Florida na kutangaza utawala wa Hispania juu ya rasi. Florida ilitawaliwa kama mkoa chini ya Ufalme Mdogo wa Hispania Mpya.

Baada ya vita ya miaka saba 1763 Hispania ilipaswa kuiachia Uingereza lakini 1783 rasi ilirudi Hispania. 1819 eneo la jimbo liliuzwa kwa Marekani.

3 Machi 1845 Florida ikawa jimbo la 27 la Marekani.

Majiji hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Majimbo ya Marekani

AlabamaAlaskaArizonaArkansasCaliforniaColoradoConnecticutDelawareFloridaGeorgiaHawaiiIdahoIllinoisIndianaIowaKansasKentuckyLouisianaMaineMarylandMassachusettsMichiganMinnesotaMississippiMissouriMontanaNebraskaNevadaNew HampshireNew JerseyNew MexicoNew YorkNorth CarolinaNorth DakotaOhioOklahomaOregonPennsylvaniaRhode IslandSouth CarolinaSouth DakotaTennesseeTexasUtahVermontVirginiaWashingtonWest VirginiaWisconsinWyoming

  Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Florida kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.