Star Tribune' (pia Star Trib au Strib, inavyoitwa mara nyingi) ni gazeti kubwa zaidi katika jimbo la Minnesota ,Marekani na huchapishwa kila siku ya wiki kama toleo la eneo la Minneapolis-Saint Paul. Toleo la Jimbo lote linaweza kupatikana Minnesota, sehemu za Wisconsin, Iowa, Dakota Kusini na Dakota Kaskazini. Gazeti shindani kubwa kabisa kwa gazeti hili ni Pioneer Press lililokuwa na makao yake St. Paul, ingawaje ,hushindana na magazeti mengine mbalimbali katika eneo lake la usambazaji.

Star Tribune
Jina la gazeti Star Tribune
Aina ya gazeti Gazeti la kila siku
Lilianzishwa 1867
Liliitwa Minneapolis Tribune
Eneo la kuchapishwa Minneapolis
Nchi Marekani Marekani
Mhariri Nancy Barnes
Mmiliki Kampuni ya Star Tribune
Mchapishaji Chris Harte
Makao Makuu ya kampuni 425 Portland Avenue
Minneapolis, Minnesota 55488
Nakala zinazosambazwa 322,362(kila siku)
534,750(Jumapili)[1]
Tovuti http://www.startribune.com/
Star Tribune Mchakato wa uchapishaji
Star Tribune Mchakato wa uchapishaji
Star Tribune Mchakato wa uchapishaji

Historia

hariri

Gazeti la leo la Star Tribune ni matunda ya muungano wa 1982 kati ya Minneapolis Star, gazeti la jioni, na Minneapolis Tribune,gazeti la asubuhi, yaliyochapishwa na kampuni moja.

Muungano kadhaa zilikuwa zimefanyika hapo awali katika miaka iliyopita,hizi zimeelezwa hapa chini. Minneapolis Tribune lilianzishwa katika mwaka wa 1867, na liliendeshwa na familia ya Murphy kati ya 1891 na 1941. Jarida la Minneapolis Journal lilianzishwa katika mwaka wa 1878 kama gazeti la jioni. Gazeti la Minneapolis Times lilikuwa gazeti la asubuhi lililoanzishwa katika mwaka wa 1899; lilinunuliwa na Tribune katika mwaka wa 1905 na jina lake likatumika kwa njia nyingi hadi mwaka wa 1948. Gazeti la Minneapolis Daily Star likaanza kuchapishwa katika mwaka wa 1920 na hapo baadaye likawa,Minneapolis Star lililosambazwa jioni.

Familia ya Cowles ilinunua Star katika mwaka wa 1935 na Journal katika mwaka wa 1939 na magazeti hayo mawili yakaunganishwa kuwa gazeti la Star-Journal. Hapo baadaye, jina lake likafupishwa kuwa gazeti la Star. Familia ya Cowles ikanunua Tribune katika mwaka wa 1941. Magazeti haya (Star na Tribune) yakaanza kuchapishwa moja la jioni na jingine la asubuhi. Katika mwaka wa 1982, majarida hayo yote yakaunganishwa kuwa 'Minneapolis Star and Tribune', na ilipofika mwaka wa 1987 gazeti likapewa jina lake la sasa la Star Tribune. Kaulimbiu ya gazeti hili ikawa "Newspaper of the Twin Cities." Katika mwaka wa 1998, Kampuni ya McClatchy ikanunua Kampuni ya Cowles Media na ikauza mali zingine zote za Cowles Media lakini ikabaki na gazeti la Star Tribune.

Katika mwaka wa 1987, jarida hili lilianza kuwa na toleo tofauti la Minneapolis ,la St.Paul na la jimbo lakini hivi sasa lina moja la Minneapolis-St. Paul na moja la habari za Minnesota kote na majimbo jirani.

Mnamo 26 Desemba 2006, Kampuni ya McClatchy iliuza jarida hili kwa kampuni ya kibinafsi ya Avista Capital Partners kwa bei ya $ milioni 530. Bei hii haikufika nusu ya bei ya $ bilioni 1.2 ambayo McClatchy ilnunua nayo Star Tribune kutoka Cowles Media.

Katika mwezi wa Machi 2007, Par Ridder alipewa cheo cha Mchapishaji katika Star Tribune baada ya mchapishaji wa zamani, J. Keith Moyer, kuacha kazi yake baada ya Star Tribune kuuzwa. Ridder alijiuzulu tarehe 7 Desemba 2007. Ridder ni mwanachama wa familia ya Ridder iliyomiliki Knight-Ridder ,wachapishaji wa magazeti kadhaa kama vile (washindani wao) Saint Paul Pioneer Press. Kuwasili kwa Ridder kulileta kesi ilipogunduliwa kuwa alikuwa ameiba kipande muhimu cha tarakilishi ya Pioneer Press cha kuhifadhi data kuhusu kampuni hiyo. Kipande hicho cha tarakilishi kilikuwa kimejaa habari kuhusu wafanyikazi wa kampuni hiyo na data ambazo Pioneer Press ilidai kuwa "siri za kibiashara". Ridder ,pia, aliajiri wafanyikazi wawili wa vyeo vya juu kutoka Pioneer Press alipoajiriwa na gazeti lile la Minneapolis. Hii ilileta ubishi kwa kuwa wafanyikazi hao wa vyeo vya juu huwa wamekatazwa ,katika mikataba yao na kampuni, kuajiriwa na kampuni zilizokuwa washindani wao kwa muda fulani. Mnamo 18 Septemba 2007, Ridder alitolewa kutoka kazi yake na hakimu wa kata la Ramsey. Hakimu huyo hamkukubalisha kufanya kazi huko tena hadi Septemba 2008.

Mnamo 1 Februari 2008, mchapishaji wa gazeti hilo alitangaza mipango ya kuuza makao makuu ya gazeti hilo yaliyokuwa Minneapolis. Mnamo 15 Januari 2009, gazeti hilo, lililokuwa la 15 kwa ukubwa katika taifa zima, lilitangaza kuwa limekuwa fukara.

Mnamo 17 Septemba 2009, Korti ya Marekani ya Bankruptcy ya Wilaya ya Kusini mwa New York ilikubali mpango maalum ya kampuni fukara. Wakopeshaji wanamiliki takriban asilimia 95 ya hisa katika kampuni hiyo ya sasa. Madeni ya kampuni sasa ni dola milioni 100, yaliyopungua kutoka madeni dola milioni 480 yaliyokuwa wakati wa kutangaza ufukara.

Usimamizi

hariri

Chris Harte ndiye mchapishaji na mwenyekiti wa sasa katika gazeti hili.

Katika mwezi wa Mei 2007, kampuni ilifanya mabadiliko katika wanahabari wake ili kuripoti zaidi habari ya Twin Cities. Ili kuleta ongezeko katika usambazaji mitaani, kulikuwa ,pia, na mpango wa kuhusisha biashara na mashirika ya ndani ya miji hiyo miwili ya Twin Cities katika kazi yao.

Kufuatia kifungu cha Mlango wa 11, katika amri za kulinda kampuni zilizokuwa na shida za kifedha, kundi lililomiliki kampuni hii,linaloongozwa na Avista Capital Partners(lililokuwa na makao yake jijini New York), halitakuwa na hisa zozote katika kampuni hiyo. Aidha, Mkurugenzi Mkuu na Mchapishaji ,Chris Harte, hataendelea kutumikia kampuni baada ya matatizo hayo kutatuliwa.

Marejeo

hariri
  1. "2008 Top 100 Daily Newspapers in the U.S. by Circulation" Archived 16 Septemba 2012 at the Wayback Machine. (PDF). BurrellesLuce. 31 Machi 2007.
  2. Ellison, Sarah (27 Desemba 2006). "McClatchy's Minneapolis Sale Aids Web Efforts". Wall Street Journal (Dow Jones & Company, Inc.): p. A3.
  3. McKinney, Matt (5 Machi 2007). "Par Ridder named Star Tribune CEO, publisher" Archived 9 Septemba 2009 at the Wayback Machine.. Minneapolis, MN: Minneapolis Star Tribune.
  4. McKinney, Matt (7 Desemba 2007). "Par Ridder resigns from Star Tribune". Star Tribune (Avista Capital Partners).
  5. Stawicki, Elizabeth (18 Septemba 2007). "Judge critical of Par Ridder's conduct in ruling" Archived 23 Januari 2010 at the Wayback Machine.. Minnesota Public Radio.
  6. McKinney, Matt (1 Februari 2008). "Star Tribune's real estate for sale". Star Tribune.
  7. Welbes, John (1 Februari 2008). "Star Tribune to put headquarters, other land up for sale". Pioneer Press.
  8. Orrick, Natasha R. (1 Februari 2008). "Star Tribune looks to sell headquarters". Minneapolis / St. Paul Business Journal. .
  9. Kary, Tiffany (16 Januari 2009). "Star Tribune Files for Bankruptcy After Ads Decline". Bloomberg.
  10. Fitzgerald, Mark (16 Januari 2009). "Economist: Avista Has Only Itself To Blame In 'Strib' Bankruptcy" Archived 17 Januari 2009 at the Wayback Machine.. Editor & Publisher (Nielsen Business Media).
  11. Pérez-Peña, Richard (16 Januari 2009). "Bankruptcy for another U.S. paper". International Herald Tribune (The New York Times Company).
  12. Newmarker, Chris (17 Septemba 2009). "Star Tribune to emerge from bankruptcy, no new publisher named". American City Business Journals, Inc..

Viungo vya nje

hariri