Stefan Bajcetic Maquieira (alizaliwa 22 Oktoba 2004) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Hispania ambaye anacheza kama beki wa kati au kiungo wa kati katika klabu ya Liverpool.

Stefan Bajcetic katika mchezo kati ya FC RB Salzburg dhidi ya Liverpool FC 27-07-2022

Maisha yake ya awali hariri

Stefan Bajcetic Maquieira[1] alizaliwa tarehe 22 Oktoba 2004[2] huko Vigo Galicia, Uhispania.Ni mtoto wa mchezaji wa mpira wa miguu wa zamani wa Serbia Srđan Bajčetić na mama mgalisia.[3][4]

Maisha ya klabu hariri

Bajcetic alitoka katika akademi ya vijana ya Celta Vigo, na alisajiliwa na klabu ya Liverpool katika Premia ligi ya Uingereza mnamo Desemba 2020..[5][6][7][8]

Maendeleo ya mchezaji huyo Bajcetic ya uwanjani yalipelekea kuongezewa mkataba mpya mnamo Agosti 2022.[9] Alipata nafasi ya kuingia kwa mara ya kwanza tarehe 27 agosti akitokea benchi pindi Liverpool ilipokuwa ikicheza na klabu ya AFC Bournemouth na Liverpool kupata ushindi wa magoli 9 kwa 0 wakiwa nyumbani Anfield.[10] Pia Bajcetic alipata nafasi ya kuingia kwa mara ya kwanza katika michuano mikubwa dunia ya UEFA walipokuwa wakicheza dhidi ya klabu ya Ajax mnamo tarehe 13 september ambapo aliingia kutoa nje katika dakika za 90 , kuchukua nafasi ya mkongwe Thiago Alcântara. [11]Kwa kufanya hivyo, akawa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi wa Liverpool kushiriki katika Ligi ya Mabingwa UEFA, na kufikia rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Billy Koumetio.[12]

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Stefan Bajcetic kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.