Sukumawiki
Sukumawiki (Brassica oleracea) | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mimea ya sukumawiki shambani
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Sukumawiki (pia: sukuma wiki) ni aina ya kabichi isiyoumba 'kichwa' na inayoliwa sana katika Afrika ya Mashariki, hususa nchini Kenya. Inatengenezwa kwa kutumia majani mabichi yanayopikwa. Lakini sukumawiki inaweza kutengenezwa pia kwa kutumia aina nyingine za majani yanayofaa kupikwa.
Jina "sukuma wiki" lamaanisha ya kwamba hii ni njia ya kula kwa siku za wiki bila gharama kubwa hadi kufikia wikendi ambako chakula bora kinapatikana - kama pesa inatosha.
Huliwa mara nyingi pamoja na ugali au chapati. Nyama, samaki au karanga inaweza kuungwa mle.
Mfano wa upishi
haririKatakata majani. Chemsha vikombe viwili vya maji katika sufuria. Ongeza majani yaliyokatwa katika maji. Ongeza chumvi na viungo vingine kama maji ya limau, nyanya na kitunguu kilichokatwa.
Unaweza kuingiza pia vipande vya nyama, samaki na karanga.
Picha
hariri-
Sukumawiki ya mawimbi
-
Maua
Viungo vya Nje
hariri- Sukuma Wiki Recipe on "allthingskenyan"
- Sukuma na nyama Archived 26 Mei 2010 at the Wayback Machine.
- Sukuma wiki: Kenyan-style sauteed greens Archived 19 Juni 2010 at the Wayback Machine.
- Sukuma wiki recipe
- Ugali and Sukuma Wiki (East African Power Lunch) Archived 8 Agosti 2011 at the Wayback Machine.