Sulkonazoli
Sulkonazoli (Sulconazole), inayouzwa kwa jina la chapa Exelderm, ni dawa inayotumika kutibu mguu wa mwanariadha, maambukizi ya fangasi kwenye ngozi, kuwashwa kwa fangasi kwenye ngozi ya sehemu za siri, mapaja ya ndani na matako (jock itch), na maambukizo ya fangasi ambayo husababisha mabaka madogo ya ngozi yaliyobadilika rangi (pityriasis versicolor).[1] Dawa hii inatumika kwa ngozi kama krimu au kioevu.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuwasha, kuchoma na uwekundu wa ngozi.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha ugonjwa wa ngozi.[1] Ni dawa ya kuzuia fangasi(antifungal) katika kundi la imidazole.[1] Inaaminika kufanya kazi kwa kubadilisha utando wa seli ya vuvu.[1]
Sulkonazoli iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1985.[1] Nchini Marekani, mrija wa gramu 60 wa dawa unagharimu takriban dola 570 za Kimarekani kufikia mwaka wa 2021.[2]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Sulconazole Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 15 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Sulconazole Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 15 Oktoba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sulkonazoli kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |