TAKILUKI
TAKILUKI (au TAKILUKIZA) ni kifupi cha Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Zanzibar. Taasisi hiyo ilianzishwa mwaka wa 1979. Inafanya kazi chini ya udhamini wa Wizara ya elimu ya Zanzibar.
Majukumu ya TAKILUKI
hariri- Kufundisha Kiswahili kwa wageni mbalimbali wanaofika Zanzibar
- Kufanya utafiti kuhusu lahaja mbalimbali na fasihi simulizi ya Kiswahili
- Kutoa mafunzo na masomo ya Kiswahili kwa watumishi wa Serikali, viongozi mbalimbali na wageni ili kukuza ujuzi wao wa lugha ya Kiswahili kwa ujumla na kuwawezesha kutumia Kiswahili fasaha
- Kutoa mafunzo ya lugha za kigeni kwa watu mbalimbali hususani wa Zanzibar
- Kukusanya na kuchambua fasihi simulizi ya visiwa vya Unguja na Pemba
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu TAKILUKI kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |