Lahaja ni vilugha vidogovidogo vya lugha moja ambavyo hubainishwa na jamii au jiografia.

Lahaja za lugha moja zinakaribiana katika matamshi, miundo ya sarufi na msamiati.

Kama lugha hutofautiana katika matamshi tu, tofauti hizo huitwa lafudhi (upekee wa uzungumzaji), si lahaja.

Uchambuzi na uchanganuzi wa lahaja ni tawi la isimujamii.

Lahaja hutofautishwa kulingana na vipengele vifuatavyo:

  1. vipengele vya sera (lahaja rasmi na lahaja sanifu)
  2. vipengele vya maoni ya wasemaji wa lugha husika
  3. vipengele vya kijamii (lahaja jamii na lahaja tabaka)
  4. vipengele vya eneo

Mfano wa lugha yenye lahaja mbalimbali ni Kiingereza na lahaja zake zinavyozungumzwa tofauti Uingereza, Marekani, Uhindi, Australia na maeneo mengine.

Lahaja za KiswahiliEdit

Lahaja za Kiswahili hutofautishwa kulingana na maeneo yake kama Kiunguja (kisiwani Zanzibar) ambacho kimekuwa msingi wa Kiswahili Sanifu, Kimvita (eneo la "Mvita" au Mombasa mjini, Kenya), ambacho zamani kilikuwa lahaja kubwa ya pili pamoja na Kiunguja, Kiamu (kisiwani Lamu, Kenya) na kadhalika. Nyingine ni pamoja na:

MarejeoEdit

  • TUKI 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  • Massamba, David 2004, "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  • Buliba, Aswani, Kimani Njogu & Alice Mwihaki 2006, "Isimujamii kwa Wanafunzi wa Kiswahili", Nairobi: The Jomo Kenyatta Foundation

Tazama piaEdit

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lahaja kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.