Taasisi ya sera za maendeleo Afrika
Taasisi ya sera za maendeleo Afrika, ni shirika lisilo la kiserikali barani Afrika liloanzishwa mwaka 2010 ili kusaidia kuondoa mipaka katika juhudi zinazowekwa ili kufanikisha maendeleo ya Afrika. Shirika lina mchango wa kutoa ushahidi ili uweze kutumika kuimarisha shughuli za kisiasa, kuhifadhi malighafi na kufanikisha utekelezaji. Lengo kuu la shirika ni kuchangia maendeleo rafiki kwa kuwezesha sera na programu tegemezi.
Kazi zao zimeainishwa katika maeneo manne. Mojawapo ya maeneo haya ni kuimarisha uwezo wa kutumia ushahidi upande wa kutunga sera. Hili ni eneo mojawapo la kazi zao ambalo linahusisha sekta za maendeleo. Wanatumia sekta tatu za maendeleo kutoa msaada wa moja kwa moja kwa watunga sera katika kuwezesha matumizi ya ushahidi, na hizi zinaunda maeneo matatu yaliyobaki ya kazi zao, ikiwa ni pamoja na: mabadiliko ya idadi ya watu na maendeleo endelevu; afya ya uzazi, mama, mtoto mchanga, na vijana; na maendeleo ya elimu na ujuzi.[1]
Marejeo
haririMakala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |