Tallinn ni mji mkuu na pia mji mkubwa wa Estonia mwenye wakazi 410,000. Iko mwambaoni wa Ghuba ya Ufini ya Baltiki na bandari yake ni bandari kuu ya nchi.

Minara ya Tallinn jinsi inavyoonekana kutoka bandari

Tallinn inajulikana kwa mji wa kale ulioingizwa na UNESCO kastika orodha la urithi wa dunia.

Historia yake ni ya karne nyingi. Kwa Zama za Kati ilikuwa mji mwanachama wa shirikisho la Hanse ijatajirika kutukana na biashara kati ya Urusi, Skandinavia na Ujerumani.

Tangu 1918 Tallinn imekuwa mji mkuu wa Estonia huria.

1940 mji pamoja na nchi yote vilivamiwa na jeshi la Kisovyeti ikawa mji mkuu wa Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiestonia hadi 1991 halafu tena mji mkuu wa Estonia huria.

Picha za Tallinn

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Estonia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tallinn kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.