Tanzania Safari Channel
Tanzania Safari Channel ni chaneli iliyo chini ya Televisheni ya Taifa ya Tanzania (TBC) iliyoanzishwa kwa lengo la kutangaza hifadhi na vivutio vya utalii nchini Tanzania.[1]
| |
Kutoka mji | Dar es salaam |
Nchi | Tanzania |
Eneo la utangazaji | Kote duniani |
Kituo kilianzishwa mwaka | 2018 |
Mwenye kituo | Televisheni ya Taifa ya Tanzania |
Tovuti | tanzaniasafarichannel.go.tz |
Tanzania Safari ilizinduliwa tarehe 15 Disemba 2018 [2][3] na waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa.
Historia
haririIlianzishwa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli alilolitoa alipozuru makao makuu ya shirika hilo Mei 16, 2019 ambapo aliagiza kuwepo kwa chaneli hiyo itakayokuwa inaonyesha vivutio vya utalii.[4]
Chaneli hii ilianzishwa kwa ushirikiano wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na wadau wengine wa utalii wakiwemo Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Mchakato wa kuanzisha chaneli hii ulihusisha pia mikutano na wadau wa sekta binafsi ambao shughuli zao zinahusiana na masuala ya utalii.
Chaneli hii inapatikana kwenye ving'amuzi mbalimbali ikiwa ni pamoja na StarTimes na Azam TV.
Marejeo
hariri- ↑ "WAZIRI MKUU, MHE. KASSIM MAJALIWA AZINDUA TANZANIA SAFARI CHANNEL | Ministry of Natural Resources and Tourism". www.maliasili.go.tz. Iliwekwa mnamo 2022-06-25.
- ↑ https://il.tzembassy.go.tz/resources/view/premier-launches-tanzania-safari-channel
- ↑ http://zanzibar24.co.tz/tbc-kuzindua-chanel-ya-utalii-tanzania-safari-channel/
- ↑ "Nukta | Majaliwa aanika faida za chaneli mpya ya utalii Tanzania". nukta.co.tz. Iliwekwa mnamo 2022-06-25.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |