Azam TV ni kampuni ya matangazo ya televisheni iliyopo nchini Tanzania na inayomilikiwa na mfanyabiashara Saidi Salim Bakhresa.

Azam TV
Ya kibiashara?Ndiyo
Aina ya tovutiking'amuzi
Kujisajirindiyo
Lugha asiliaKiswahili
MmilikiAzam TV
MwanzilishiSaidi Salim Bakhresa
Imeanzishwa na2013

Kampuni ilianzishwa mwaka 2013 jijini Dar es Salaam, Tanzania. Makao makuu yake yapo Tazara, barabara ya Nyerere.

Kampuni hiyo inarusha matangazo yake katika nchi za Afrika mashariki na ya kati (Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Malawi n.k.).

Kupitia king'amuzi chake kimesheheni chaneli kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni katika vipengele kama chaneli za watoto, wanyama, michezo, habari, miziki n.k. pia kuna chaneli za redio.

Mwaka 2023 Azam TV inatimiza miaka kumi, hivyo wanasherehekea kwa kufanya shuguli mbalimbali kama vile uzinduzi wa matawi na kutoa misaada mbalimbali.

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Azam TV kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.