Tatyana Marisol Ali (alizaliwa mnamo 24 Januari 1979) ni mwigizaji wa filamu na mwimbaji wa muziki wa R&B kutoka nchini Marekani. Huenda akawa anafahamika zaidi kwa kucheza kama Ashley Banks kutoka katika ucheshi wa Fresh Prince of Bel-Air, aliokuwa anaigiza na Will Smith.

Tatyana Ali
Tatyana Ali at the U.S. Presidential Inauguration (2009).
Tatyana Ali at the U.S. Presidential Inauguration (2009).
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Tatyana Marisol Ali[1]
Amezaliwa 24 Januari 1979 (1979-01-24) (umri 45)
Asili yake North Bellmore, Long Island, New York, Marekani
Aina ya muziki R&B, Soul, Dansi-Pop
Kazi yake Filamu, Mwigizaji wa televisheni
Mwimbaji
Miaka ya kazi 1985 — hadi leo (mwigizaji)
1997 — hadi leo (mwibaji)
Studio MJJ/Work/SME Records
(1997—2001)
Ame/Wameshirikiana na Will Smith
Tovuti tatyanaalionline.com

Wasifu

hariri

Maisha ya awali

hariri

Ali alizaliwa mjini Long Island, New York, Marekani, ni binti wa Sonia, mwuguzi, na Sheriff Ali, askari mpelelezi. Mama yake ni mzaliwa wa Panama na baba yake ni mhindi asilia kutoka Trinidad na Tobago. Ali pia ana wadogo zake wa kike wawili, mmoja anaitwa Anastasia mwingine anaitwa Kimberly. Ali ni mwongeaji mzuri wa Kiingereza na Kihispania.

Tatyana alipata elimu yake ya sekondari katika shule ya Marymount High School iliyopo magharibi mwa Los Angeles, California, na Buckley School iliyopo Sherman Oaks, Los Angeles, California. Mnamo mwaka wa 2002, Ali alihitimu Chuo Kikuu cha Harvard (Harvard University) na kupata digrii ya sayansi ya jamii.

Filamu alizoigiza Ali

hariri
Mwaka Filamu Aliigiza kama Maelezo
1987 Eddie Murphy Raw Dada yake Eddie Kipande kifupi
1988 Crocodile Dundee II Park Girl
1988 Wow, You're a Cartoonist! Child Cartoonist Filamu fupi
1997 Fakin' da Funk Karyn
1997 Kiss the Girls Janell Cross
1998 The Clown at Midnight Monica
1999 Jawbreaker Brenda
2000 Brother Latifa
2001 The Brothers Cherie Smith
2003 National Lampoon Presents Dorm Daze Claire
2004 Nora's Hair Salon Lilleana
2005 Back in the Day Alicia Packer
2005 Domino One Laeticia Richards
2006 Glory Road Tina Malichi
2006 A Warm Place Clair Andrews Filamu fupi
2007 The List Cynthia
2008 Down & Out Filamu fupi
2008 Nora's Hair Salon 2: A Cut Above Lilleana
2008 Hotel California Jessie
2009 Mother and Child Maria
2010 Pete Smalls Is Dead Cocktail Waitress
2012 Privileged Talia
2012 Dysfunctional Friends Alex
2012 Home Again Marva Johnson
2013 24 Hour Love Simply
2013 The Last Letter Jillian
2014 Locker 13 Lucy
2015 November Rule Leah

Almbamu alizotoa

hariri
  • Kiss the Sky (1998)
  • The Light (2007)

Nyimbo maarufu

hariri
  • "Daydreamin'" - #5 US, #6 UK
  • "Boy You Knock Me Out" (Akishirikiana na Will Smith) - #3 UK
  • "Everytime" - #20 UK
  • "It's All Right"/"Somebody Loves You" - Bado kutolewa.

Marejeo

hariri
  1. "Tatyana Ali at NNDB". NNDB.com. Iliwekwa mnamo 2007-09-24.

Viungo vya nje

hariri


  Makala hii kuhusu muziki wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tatyana Ali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.