Willard Christopher "Will" Smith, Jr. (amezaliwa tar. 25 Septemba 1968)[1] ni mwigizaji, mtayarishaji wa filamu, na rapa kutoka nchini Marekani. Amefurahia sana mafanikio yake ya kimuziki, televisheni na filamu. Gazeti la "Newsweek" limemwita mwigizaji mwenye uwezo mkubwa kabisa duniani.[2] Smith amewahi kushindanishwa kwenye tuzo za Golden Globe mara nne, Academy Awards mara mbili, na ameshinda matuzo kede-kede ya Grammys.

Will Smith

Will Smith mnamo 2019
Amezaliwa Willard Christopher Smith, Jr.
25 Septemba 1968 (1968-09-25) (umri 55)
Wynnefield, Philadelphia, Pennsylvania, West Philadelphia, Pennsylvania, U.S.
Kazi yake Mwigizaji, rapa, mtayarishaji wa filamu, mtayarishaji wa rekodi, mtayarishaji wa televisheni
Miaka ya kazi 1987–hadi leo
Ndoa Sheree Zampino (1992–1995)
Jada Pinkett Smith (1997–hadi leo)
Tovuti rasmi

Smith ameanza kujibebea umaarufu akiwa kama rapa chini ya jina la The Fresh Prince mwishoni mwa miaka ua 1980 na jina la uhusika kwenye mfululizo wa televisheni wa The Fresh Prince of Bel-Air. Filamu maarufu ambazo kacheza ni pamoja na Bad Boys na mfululizo wake wa pili Bad Boys II; Men in Black na mfululizo wake wa pili Men in Black II; Independence Day; I, Robot ; Ali; The Pursuit of Happyness; I Am Legend; Hancock; na Seven Pounds. Yeye ni mwigizaji pekee katika historia kuwa na mfululizo wa filamu nane zilizopata mauzo ya dola za Kimarekani milioni 100 kwenye sanduku la ofisi la nyumbani na vilevile kuwa kama mwigizaji pekee kuwa na filamu nane mfululizo kushika nafasi ya kwanza kwenye siku ya uzinduzi wa nyumbani akiwa kama mwigizaji kiongozi.[3]

Familia na maisha ya mwanzoni hariri

Smith, ni Mwafrika-Mwamerika aliyezaliwa na kukulia mjini West Philadelphia na Germantown huko Northwest Philadelphia. Mama yake, Caroline, alikuwa msimamizi wa shule ambaye alifanya kazi kama msimamizi wa bodi ya shule Philadelphia, na baba yake, Willard Christopher Smith, Sr., alikuwa mhandisi wa majokofu.[4][5] Kiimani, alilelewa Kibaptist.[6] Wazazi wake walitengana akiwa na umri wa miaka kumi na tatu na kuja kupeana talaka rasmi akiwa na umri wa miaka thelathini na mbili.[7] Ucheshi wa Smiths na jinsi anavyoonekana akiwa shuleni, wakampa jina la utani kama "Prince", ambalo hatumaye likaja kugeuka na kuwa "Fresh Prince". Wakati yuujanani mwake, Smith akaanza kurao na hatimaye akaanza kushirikiana na Jeff Townes (a.k.a. DJ Jazzy Jeff), ambaye alikutana naye kwenye sherehe moja hivi. Akanza kuhudhuria kwenye shule ya Overbrook High School ya mjini West Philadelphia. DJ Jazzy Jeff & The Fresh Prince ilizaliwa na Smith huku yeye akiimba mistari wakati Townes anashughurikia suala zima la kusugua na kuchanganya midundo—mwungano huo ulikuwa gumzo sana kwenye nyanja za muziki wa hip hop hasa katika miaka ya 1980 na mwazoni mwa 1990.

Diskografia hariri

Filmografia hariri

Mwaka Filamu Uhusika Mshahara (US$)[8] Maelezo
1990 Saturday Morning Videos Host TV
ABC Afterschool Special - "The Perfect Date" Hawker TV
The Fresh Prince of Bel-Air William "Will" Smith TV (1990-1996)
1992 Blossom Fresh Prince TV, Kauza sura
Where the Day Takes You Manny 50,000
1993 Made in America Tea Cake Walters 100,000
Six Degrees of Separation Paul 500,000
1995 Bad Boys Detective Mike Lowrey 2,000,000
1996 Independence Day Captain Steven "Steve" Hiller, USMC 5,000,000
1997 Men in Black James Darrell Edwards / Agent J 5,000,000
1998 Enemy of the State Robert Clayton Dean 14,000,000 Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture
1999 Torrance Rises Kauza sura
Wild Wild West Captain James "Jim" West 7,000,000
2000 Welcome to Hollywood Yeye mwenyewe
The Legend of Bagger Vance Bagger Vance 10,000,000 Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture
2001 Ali Muhammad Ali 20,000,000 Kashindanishwa — Academy Award for Best Actor
Kashindanishwa — Broadcast Film Critics Association Award for Best Actor
Kashindanishwa — Golden Globe Award for Best Actor – Motion Picture Drama
Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture
2002 Men in Black II James Darrell Edwards / Agent J 20,000,000
+ 10% ya mapato ya filamu
BET Award for Best Actor
Kashindanishwa — Black Reel Awards of 2002
Girlfriend ya B2K Yeyey mwenyewe Muziki wa video
2003 Bad Boys II Detective Mike Lowrey 20,000,000
+ 20% ya mapato yote ya filamu
Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture
2004 A Closer Walk Mwadithiaji Makala
Jersey Girl Yeye mwenyewe Kauza sura tu
American Chopper Yeye mwenyewe TV, Kauza sura
I, Robot Detective Del Spooner 28,000,000 Mtayarishaji
Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture
Shark Tale Oscar 15,000,000 Sauti
2005 There's a God on the Mic Makala
Hitch Alex "Hitch" Hitchens 20,000,000 BET Award for Best Actor
Kashindanishwa — Black Movie Award for Best Actor
Kashindanishwa — Black Reel Awards of 2006
Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture
2006 The Pursuit of Happyness Chris Gardner 10,000,000
+ 20% of the gross
Mtayarishaji

Kashindanishwa— Academy Award for Best Actor
Kashindanishwa — Black Reel Awards of 2007
Kashindanishwa — Broadcast Film Critics Association Award for Best Actor
Kashindanishwa — Chicago Film Critics Association Award for Best Actor
Kashindanishwa — Golden Globe Award for Best Actor – Motion Picture Drama
Kashindanishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture
Kashindanishwa — Screen Actors Guild Award for Outstanding Performance by a Male Actor in a Leading Role

2007 I Am Legend Dr. Robert Neville 25,000,000 Mtayarishaji, Kashindanishwa — BET Award for Best Actor
Kashindenishwa — NAACP Image Award for Outstanding Actor in a Motion Picture
2008 Hancock John Hancock 20,000,000
+ 20% ya mapato ya filamu
Mtayarishaji
Lakeview Terrace Mtayarishaji
The Secret Life of Bees Mtayarishaji
Seven Pounds Tim Thomas Mtayarishaji
2009 The Mark[9]
Unbroke: What You Need to Know About Money Television special
2010 Time Share[10]
2011 I Am Legend: Awakening[11][12] Robert Neville
2012 Men in Black III[13] James Darrell Edwards / Agent J

Soma zaidi hariri

Marejeo hariri

 1. Jason Ankeny (2008). "Will Smith on MSN". MSN. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-01-11. Iliwekwa mnamo 2008-07-17. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
 2. Sean Smith. "The $4 Billion Man", Newsweek, 2007-04-09. Retrieved on 14 Februari 2009. Archived from the original on 2010-01-06. 
 3. "WEEKEND ESTIMATES: 'Hancock' Delivers $107M 5-Day Opening, Giving Will Smith a Record Eighth Consecutive $100M Grossing Movie!; 'WALL-E' with $33M 3-Day; 'Wanted' Down 60 Percent for $20.6M; 'Kit Kittredge' a Disaster!". Fantasy Moguls. 2008-07-03. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-07-06. Iliwekwa mnamo 2008-07-07.
 4. Will Smith Biography (1968-)
 5. "Where there's a Will, there's a way", Taipei Times, 2004-08-09. 
 6. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-12-19. Iliwekwa mnamo 2009-10-21.
 7. Rebecca Winters Keegan. "The Legend of Will Smith", Time, 2007-11-29. Retrieved on 2009-10-21. Archived from the original on 2007-12-01. 
 8. http://www.the-numbers.com/people/WSMIT.php
 9. http://www.boxofficeprophets.com/tickermaster/listing.cfm?tmID=1216
 10. http://www.the-numbers.com/movies/2010/TMSHR.php
 11. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-05-27. Iliwekwa mnamo 2009-10-21.
 12. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-22. Iliwekwa mnamo 2009-10-21.
 13. Brendon Connelly (21 Aprili 2010). "Barry Sonnenfeld Confirms Will Smith and Tommy Lee Jones For Men in Black 3D". /Film. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-19. Iliwekwa mnamo 20 Aprili 2010.

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Will Smith kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.