Tenth Avenue North


Tenth Avenue North ni bendi la Marekani linaloimba nyimbo za Kikristo za kisasa. Bendi hili hutoka eneo la West Palm Beach, Florida. Bendi hili hushirikisha Mike Donehey(mwimbaji na mchezaji gitaa) , Jeff Owen (mchezaji gitaa ya kutumia umeme na mwimbaji msaidizi), Jack Jamison (mchezaji ngoma) na Scott Sanders (mchezaji gitaa ya aina ya bass).

Tenth Avenue North

Maelezo ya awali
Asili yake West Palm Beach Florida
Marekani Marekani
Aina ya muziki Nyimbo za Kikristo za kisasa
Miaka ya kazi 2002 hadi sasa
Studio Reunion Records
Tovuti http://www.tenthavenuenorth.com/
Wanachama wa sasa
Mike Donehey
Jeff Owen
Scott Sanders
Jason Jamison

Albamu yao ya kwanza , Over and Underneath, ilitolewa mnamo 20 Mei 2008 na studio ya Reunion Records, na ,karibu na wakati huo, bendi hili lilienda ziara ya kupigia debe albamu yao. Wimbo wao wa Love Is Here uliorodheshwa katika chati ya nyimbo bora 20 katika chati ya muziki ya Kikristo ya Marekani ya U.S. Contemporary Christian Music na uka fika #3 mnamo 21 Juni 2008. Wimbo huo ulimaliza mwaka wa 2008 kama wimbo wa 12 katika orodha ya nyimbo zinazochezwa sana katika stesheni ya redio ya Christian Hit Radio, hii orodha ilichapishwa na gazeti la R&R.

Wimbo wao mwigine wa By Your Side ulitolewa mwishoni mwa mwezi wa Agosti 2008 na ,hatimaye, ukawa #1 katika stesheni ya Christian Hit Radio katika mwaka wa 2009. Kulingana na chati ya R&R, wimbo huo ulibaki katika nafasi hiyo kwa wiki tatu mpaka 13 Februari 2009.

Bendi hilo limezuru na Bendi la David Crowder na MercyMe ,pia, limezuru likiwa pekee yake kote Marekani. Walishinda tuzo ya "Waimbaji Wapya wa Mwaka" katika Tuzo za 40 za GMA Dove katika mwezi wa Aprili 2009.

Wanachama

hariri

Wanachama wa sasa

hariri
  • Mike Donehey - mwimbaji kiongozi, mchezaji gitaa
  • Jeff Owen - mchezaji gitaa, mwimbaji
  • Jason Jamison - mchezaji ngoma

Wanachama wa zamani

hariri
  • Scott Sanders - mchezaji gitaa ya aina ya bass, mchezaji piano.
  • 2009: Tuzo ya GMA Dove ya Waimbaji Wapya wa Mwaka(washindi).

Diskografia

hariri

Albamu

hariri

Albamu za Kujitegemea

hariri
  • 2002: Broken Down (albamu ya kurekodi wakijitegemea)
  • 2003: Don't Look Back (albamu ya kurekodi wakijitegemea)
  • 2005: Speaking of Silence (albamu ya kurekodi wakijitegemea)
  • 2006: God With Us EP (albamu ya kurekodi wakijitegemea)
  • 2008: Over and Underneath (Walirekodi na Studio za Reunion Records) Marekani # 118

Albamu za Studio

hariri
Mwaka Maelezo ya albamu # ya juu kabisa kwenye chati Mauzo
Marekani Marekani
Rock
Marekani
Kikristo
2008 Over and Underneath

95 37 2
  • Mauzo Marekani: 100,000+

Nyimbo zisizokuwa kwa albamu

hariri
  • Love is Here
  • By Your Side - #1 kwa wiki tatu katika mwezi wa Februari 2009, uliorodheshwa katika Nyimbo Bora 30 za 2008 katika chati ya Air 1.
  • Hold My Heart

Virejeleo

hariri
  1. ^ Tenth Avenue North’s Debut Single Love Is Here Breaks...; CCM magazine; Ilihifadhiwa 23 Machi 2008 kwenye Wayback Machine. 13 Machi 2008;
  2. ^ Contemporary Christian Music Chart for R&R magazine as reported at the Weekend 22; 21 Juni 2008; Retrieved 22 Juni 2008
  3. ^ 2008 Year End Charts/Top Christian CHR songs, Ilihifadhiwa 25 Mei 2009 kwenye Wayback Machine. R&R magazine,
  4. ^ "Christian CHR National Airplay". Ilihifadhiwa 14 Oktoba 2008 kwenye Wayback Machine. R&R. 2009-02-13
  5. ^ "2009 Winners". Doveawards.com. Ilihifadhiwa 27 Aprili 2009 kwenye Wayback Machine.

Viungo vya nje

hariri