Terconazole, inayouzwa kwa jina la chapa Terazol miongoni mwa zingine, ni dawa inayotumika kutibu maambukizi ya kuvu ukeni,[1] na ni matibabu ya mstari wa kwanza kwa matumizi haya.[1] Dawa hii inatumika ndani ya uke kama losheni au tembe ya kuweka ukeni.[1]

Terconazole
Jina la Utaratibu la (IUPAC)
1-[4-[ [(2S,4S)-2-(2,4-Dichlorophenyl)-2-(1,2,4-triazol-1-ylmethyl)-1,3-dioxolan-4-yl]methoxy]phenyl]-4-propan-2-yl-piperazine
Data ya kikliniki
Majina ya kibiashara Terazol
AHFS/Drugs.com Monograph
MedlinePlus a688022
Kategoria ya ujauzito ?
Hali ya kisheria ?
Data ya utendakazi
Kufunga kwa protini 94.9%
Vitambulisho
Nambari ya ATC ?
Data ya kikemikali
Fomyula C26H31Cl2N5O3 
 N(hii ni nini?)  (thibitisha)

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuwasha, maumivu ya tumbo na hedhi chungu.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha athari za mzio.[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[2] Dawa hii inafanya kazi kwa kuvuruga utando wa seli ya kuvu fulani.[1] Ina wigo mpana wa shughuli za kitiba.[1]

Terconazole iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1987[1] na inapatikana kama dawa ya kawaida.[3] Nchini Marekani, bomba moja linagharimu takriban dola 20 za Kimarekani.[3]

Marejeleo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 "Terconazole Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 29 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "AHFS2021" defined multiple times with different content
  2. "Terconazole topical Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 29 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 "Terconazole Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Oktoba 2016. Iliwekwa mnamo 29 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)