Terror Squad
Kwa matumizi mengine, angalia Terror Squad (maana)
Terror Squad | |
---|---|
Logo yao
| |
Maelezo ya awali | |
Asili yake | The Bronx, New York |
Aina ya muziki | Gangsta rap Latino rap Hardcore rap East Coast Rap |
Miaka ya kazi | 1999 - hadi leo |
Studio | Koch Records Terror Squad Entertainment |
Wanachama wa sasa | |
Fat Joe Pistol Pete Cool & Dre Kill All Rats Mafia O.Z. H Mob The Leader Nu Jerzey Devil | |
Wanachama wa zamani | |
DJ Khaled Big Pun Cuban Link Triple Seis Prospect Tony Sunshine Remy Ma Armageddon |
Terror Squad ni kundi la muziki wa hip hop na pia studio kutoka mjini Bronx, New York, ambalo lilianzishwa mnamo mwaka 1998 kwa kupitia kibao kimoja mashuhuri kinachotoka katika albamu ya Don Cartagena ya mwimbaji kiongozi wa kundi hilo Fat Joe.
Walitoa albamu yao ya kwanza iliyojulikana kwa jina la Terror Squad, kunako 1999, ikiwa imeambatana na kibao chao cha kwanza kilichokwenda kwa jina la "Whatcha Gon' Do", ambacho kiliimbwa zaidi na Big Punisher, ambaye alifariki dunia kwa tatizo la ugonjwa moyo manmo mwa 2000. Baada ya kifo cha Big Pun, washikaji zake wa toka kitambo Bw. Cuban Link na Triple Seis, wakajitoa katika kundi na badala yao nafasi hizo zikawa nimeshikiliwa na Remy Martin na Tony Sunshine.
Kama jinsi vile kundi lilivyo simama kwa kufuatia kifo cha Big Pun, wanachama wengi wa kundi hilo wakaangukia katika fumbo zito kwa kufuatia mafanikio makubwa alioyoyapata rapa mwenzao Fat Joe, akiwa kama msanii wa kujitegea na kuwashinda hata wale wenzake.
Kundi lilirudi tena ulingoni na wakafanikiwa kutoa albamu yao ya pili iliyokwenda kwa jina la True Story, mnamo mwaka wa 2004. Albamu ilibeba byimbo maarufu ya "Lean Back," ambayo ilitayarishwa na Scott Storch, na kuweza kushika nafasi ya kwanza katika chati za Billboard Hot 100 bora na nafasi ya 24 katika UK.[1]
Muziki
haririAlbum
hariri- Terror Squad - The Album
- Imetolewa: 21 Septemba 1999
- Chati iliyoshika: #22 US
- Maelezo ya RIAA: -
- Single: Whatcha Gon Do
- True Story
- Imetolewa: 27 Julai 2004
- Chati iliyoshika: #24 US
- Maelezo ya RIAA: Gold
- Single: Lean Back, Take Me Home, Yeah Yeah Yeah
- New Story
- Imepangiliwa:2008
- Chati iliyoshika: HKN
- Maelezo ya RIAA:
- Single: Hamna
Marejeo
hariri- ↑ Terror Squad Wamesaini Mkataba Mpya na Studio ya Koch Records Archived 5 Juni 2008 at the Wayback Machine.. Boombox.co.uk: Okt. 23, 2007
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Terror Squad kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |