The Bridges of Madison County


The Bridges of Madison County ni Riwaya iliyoweza kufanya vizuri katika mauzo kwa mwaka 1992, iliyoandikwa na mwandishi wa Kimarekani anayefahamika kwa jina la Robert James Waller.

The Bridges of Madison County  
Faili:BridgesOfMadisonCounty.jpg
Mwandishi (wa){{{mwandishi}}}
ISBNISBN:
OCLC Number24246926
Dewey Decimal813/.54 20
LC ClassificationPS3573.A4347 B75 1992

Riwaya hii inahadithia maisha ya mwanamke aliyeolewa na mwenye asili ya Italia aliyeishi maisha ya upweke katima mika ya 1960 katika eneo lililofahamika kama Madison County, Iowa, ambaye baadae alikuja kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na mpiga picha wa National Geographic kutoka eneo la Bellingham, Washington , ambaye alitembelea eneo la Madison Country kwa ajili ya kutengeneza hadithi ya picha katika madaraja yaliyofahamika kama Covered Bridge. Hadithi hiyo inasimuliwa na kuibua hisia kama vile ni hadithi ya ukweli, lakini katika hali ya uhalisia, si hadithi ya uhalisia na matukio yote yamebuniwa. Hata hivyo, mwanzoni mwa riwaya hiyo, mwandishi ameanza kwa mahojiano ambayo yanaelekea kuonesha uhusiano mkubwa baina ya mhusika mkuu wa riwaya hiyo na mwandishi mwenyewe. [1] Riwaya hii ni moja kati riwaya ambazo zimeweza kufanya vizuri kwa upande wa mauzo kwa karne ya ishirini na moja, kwa kufanikiwa kuuza zaidi ya nakala milioni hamsini dunia nzima

Awali, riwaya hii ilichapishwa nchini Uingereza ikiwa na jina la Love in Black and White.[2] Riwaya ya Bridges of Madison County ilitengenezwa katika filamu mwaka 1995, filamu iliyobeba jina hilo hilo, filamu ikiongozwa na Clint Eastwood. Hadithi fupi ilinayoandikwa mwishoni mwa kitabu, iliyoitwa A Thousand Country Roads ilichapishwa mwaka 2022. Hii ilitoa mwendelezo wa maisha ya wahusika wawili baada ya mahusiano yao ya kimapenzi yaliyodumu kwa siku nne. Hawakuweza kukutana tena wakiwa duniani lakini maisha yao yaliendelea kuwa pamoja hadi kifo.

Kwa mujibu wa San Francisco Chronicle, riwaya hii anaielezea kuwa ya ushairi, yenye kuibua hisia na ya kusisimua juu ya upendo usiokuwa na mwisho.

Marejeo

hariri
  1. Transcript of interview with Robert James Waller at http://www.readinggroupguides.com/guides3/thousand_country_roads2.asp#bio Ilihifadhiwa 13 Mei 2013 kwenye Wayback Machine., retrieved 4 Feb, 2008
  2. Love in Black and White, paperback, Mandarin, 1993.

Viungo vya nje

hariri