Tiktok

video inayolenga mitandao ya kijamii na huduma ya mitandao ya kijamii inayomilikiwa na ByteDance

Tiktok (huko China inajulikana kama Douyin; kwa Kichina: 抖音; pinyin: Dǒuyīn) ni mfumo wa utangazaji wa video fupi unaomilikiwa na kampuni ya Kichina ya ByteDance[1]. Huandaa na kutengeneza aina mbalimbali za video za watumiaji wake katika muundo wa video fupi zenye dhamira tofautitofauti kama vile mizaha, vichekesho, hila, ucheshi, kucheza na burudani[2] [3] kwa muda wa sekunde 15 hadi dakika 10.

ikon ya TikTok kwa maneno

Tiktok ni toleo la Douyin ambalo liliachiwa sokoni mnamo Septemba 2016. Tiktok ilizinduliwa mnamo 2017 kwa iOS na Android kwenye masoko nje ya China. Hata hivyo, ilipatikana duniani kote baada tu ya kuunganishwa na huduma nyingine ya mitandao ya kijamii ya China, Musical.ly, tarehe 2 Agosti 2018.

TikTok na Douyin ni mifumo inayofanana kwa mtumiaji lakini haina ufikiaji sawa kimaudhui. Pia huduma zao na programu husika zinapatikana kwenye soko. Bidhaa hizo ni sawa ijapokuwa sifa zao zinatofautiana. Douyin inajumuisha mfumo wa utafutaji wa ndani wa nyuso za watu kwenye video zao na vipengele vingine kama vile kununua,kuweka nafasi kwenye hoteli na kufanya hakiki zenye lebo ya kijiografia. Tangu kuzinduliwa mwaka 2016, Tiktok and Douyin zilipata umaarufu kwa kasi karibu sehemu zote duniani.Tiktok ilipata zaidi ya wapakuaji billioni 2 duniani kote mwezi octoba 2020.Morning Consult iliorodhesha TikTok kama chapa ya tatu inayokua kwa kasi zaidi 2020, Baada tu ya Zoom na Peacock. Cloudflare iliorodhesha TikTok kama tovuti maarufu ya 2021 kuzidi Google.

Tiktok imesemekana kuwa chanzo cha athari za kisaikolojia kama vile uraibu pamoja na mabishano kuhusu maudhui yasiyofaa, taarifa potofu, udhibiti na faragha ya mtumiaji.

Historia hariri

TikTok ni jukwaa la kijamii la video ambalo lina watumiaji wengi duniani kote. Historia yake inaanza na maendeleo ya jukwaa la awali lililokuwa likijulikana kama Douyin nchini China. Douyin lilizinduliwa na kampuni ya Kichina ByteDance mnamo Septemba 2016. Baadaye, ByteDance iliamua kuzindua toleo la kimataifa la Douyin chini ya jina la TikTok mnamo Septemba 2017.

TikTok ilipata umaarufu haraka kutokana na mfumo wake wa ubunifu wa kushiriki video fupi, kawaida zikiwa chini ya sekunde 60, na inayomruhusu mtumiaji kutumia vichujio, athari za sauti, na zana zingine za ubunifu. Jukwaa hili limekuwa maarufu hasa kati ya kizazi cha vijana.

Ukuaji wa TikTok umesababisha changamoto kadhaa, pamoja na masuala ya faragha, utawala wa data, na wasiwasi wa usalama wa kitaifa katika baadhi ya nchi. Hata hivyo, jukwaa hilo limeendelea kuwa maarufu, likichangia kwa kiasi kikubwa kwenye utamaduni wa mtandaoni na kuleta umaarufu kwa watumiaji wake, maarufu na wasio maarufu sawa na vile inavyotumiwa kama jukwaa la kujitokeza kwa talanta mbalimbali.

Tanbihi hariri