Titus Naikuni

Titus Naikuni ni Mkurugenzi na Naibu Mkuu wa Kundi la Kenya Airways.. Tito ana shahada ya Sayansi na Digirii ya hueshima katika Mechanical Engineering kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.Yeye pia ni mhitimu wa Shule ya Biashara ya Harvard katika programu ya Usimamizi wa Mpango wa Maendeleo (PMD71) na alipatiwa Shahada ya Daktari katika Uhandisi na Sayansi na Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta tuzo ya kutambua mchango wake kwa maendeleo. Yeye alijiunga Magadi Soda Company mwaka 1979 kama mhandisi wa kujifunza na kupanda hadi nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa kampuni mwaka 1995 na Mkurugenzi Mkuu wa Magadi Railway Company (kiungo cha Magadi Soda Company) mwaka 1996.

Titus Naikuni

Kati ya Agosti 1999 na Machi 2001, Titus alikuwa mwanachama wa timu ya wajuzi wakenya waliodhaminiwa na Benki kuu ya Dunia, iliojulikana kama "Dream Team" ambao walikuwa wanaohusishwa na Serikali kugeuza uchumi wa Nchi. Katika uwezo huu Titus aliwahi kuwa katibu wa kudumu katika Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano na alikuwa mjumbe wa Bodi ya Kenya Airways. Alirudi Magadi Soda Company Aprili 2001 ambapo aliendelea kutumikia kama Mkurugenzi, nafasi aliyoitumikia hadi alipoajiriwa na Kenya Airways mwezi Februari 2003. Titus amekuwa na uzoefu mkubwa wa Bodi baada ya kuwa mjumbe katika bodi za kampuni mbalimbali pamoja kama mwanachama wa bodi ya Brunner Mond (Afrika ya Kusini), kama Mwenyekiti wa Kenya Power & Lighting Company na kama Mwenyekiti wa Housing Finance Company Limited. Yeye alipokea tuzo la Meneja wa Mwaka nchini Kenya mwaka 2002. [1]

Mnamo Septemba 2006, Titus Naikuni aliteuliwa Mwenyekiti wa Tume ya Filamu ya Kenya [2]

Sasa yeye ni mjumbe wa bodi za Maersk Kenya Ltd, Access Kenya Ltd, CFC Bank Kenya Limited, makamu Mwenyekiti wa Magadi Soda Company Ltd na mwanachama wa Baraza la Ushauri Unilever Afrika.

Angalia PiaEdit