Tiva-chati
Tiva-chati | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mchoro wa tiva-chati
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Tiva-chati (Lanioturdus torquatus) ni ndege mdogo wa familia Platysteiridae. Anatokea Angola na Namibia tu katika pori yenye miti ya miiba. Hutavuta chakula ardhini mpaka sm 25 juu katika uoto; hula wadudu. Tago lake hutengenezwa kwa umbo wa kikombe katika mgunga mfupi. Jike huyataga mayai 2-3.