Tonino Valerii (amezaliwa tar. 20 Mei 1934) ni mwongozaji wa filamu wa Kitaliano, anafahamika zaidi kwa kuongoza filamu za western, maarufu kama Spaghetti Western. Valerii alianza shughuli za filamu akiwa kama mwongozaji msaidizi wa Sergio Leone, alimsaidia kuongoza filamu ya A Fistful of Dollars, kabla ya kuhama na kuanza kuongoza filamu zake mwenyewe. Miongoni mwa filamu zake zenye kufahamika zaidi ni kama ifuatavyo: Day of Anger (1968) The Price of Power (1969), A Reason to Live, a Reason to Die (1972) na My Name Is Nobody (1973), iliyochezwa na Henry Fonda.

Ona pia

hariri

Viungo vya nje

hariri