Anthony Howard "Tony" Goldwyn (amezliwa tar. 20 Mei 1960) ni mwigizaji na mwongozaji wa filamu kutoka nchini Marekani. Amepata umaarufu zaidi kwa kucheza kama adui Carl Bruner kwenye filamu ya Ghost, Colonel Bagley kwenye The Last Samurai, na sauti ya Tarzan kwenye katuni ya Disney Tarzan.

Tony Goldwyn

Goldwyn mnamo Mei 2014
Amezaliwa Anthony Howard Goldwyn
20 Mei 1960 (1960-05-20) (umri 64)
Los Angeles, California, US
Kazi yake Mwigizaji/Mwongozaji
Miaka ya kazi 1986–present

Maisha binafsi

hariri

Goldwyn alizaliwa mjini Los Angeles, California, akiwa kama mtoto wa Jennifer Howard na mtayarishaji wa filamu Samuel Goldwyn, Jr. - babu zake Goldwyn walikuwa vigogo wa filamu ambaye ni Samuel Goldwyn na mwigizaji filamu wa kike Bi. Frances Howard,[1] wakati wazee wa babu yake walikuwa watunzi wa tamthilia Sidney Howard na mwigizaji wa kike Clare Eames. Goldwyn alihitimua elimu yake ya juu katika chuo cha Hamilton College cha mjini Clinton, New York, Chuo Kikuu cha Brandeis huko mjini Waltham, Massachusetts (ambamo alipata shahada moja ya sanaa ya uchoraji), na baadaye London Academy of Music and Dramatic Art. Goldwyn amemwoa msanifu utayarishaji Jane Musky. Wawili hao wana mabinti wawili, Anna na Tess.

Filamu

hariri
  • Friday the 13th Part VI: Jason Lives (1986)
  • Gaby: A True Story (1987)
  • Ghost (1990)
  • Kuffs (1991)
  • Traces of Red (1992)
  • The Pelican Brief (1993)
  • Nixon (1995)
  • Reckless (1995)
  • Trouble on the Corner (1997)
  • Kiss the Girls (1997)
  • The Lesser Evil (1998)
  • A Walk on the Moon (1999)
  • Tarzan (1999) (sauti)
  • Pocahontas: The Legend (1999)
  • The 6th Day (2000)
  • An American Rhapsody (2001)
  • The Song of the Lark (2001)
  • Bounce (2000)
  • Joshua (2002)
  • Kingdom Hearts (2002) (sauti ya Tarzan)
  • The Last Samurai (2003)
  • Without a Trace (2004)
  • The Godfather of Green Bay (2005)
  • The Last Kiss (2006) (director)
  • Grey's Anatomy (2006) (mtayarishaji wa vipindi viwili)
  • Dexter (2006)
  • Private Practice (2007)
  • The Last House on the Left (2009)
  • The Good Wife (2009)
  • Conviction (2010) (mtayarishaji)
  • Promises, Promises (2010)
  • The Mechanic (2011)
  • Scandal (2012)

Marejeo

hariri
  1. "JewishJournal.com". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-08. Iliwekwa mnamo 2010-04-08.

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: