Ghost ni filamu ya drama na njozi ya mwaka wa 1990. Ndani yake anakuja Patrick Swayze, Demi Moore, Tony Goldwyn na Whoopi Goldberg, imetungwa na Bruce Joel Rubin na kuongozwa na Jerry Zucker. Ilichaguliwa kedekede na Academy Awards, ikiwa ni pamoja na Filamu Bora, na kushinda Best Original Screenplay, vilevile Best Supporting Actress imekwenda kwa Whoopi Goldberg.

Ghost
Imeongozwa na Jerry Zucker
Imetayarishwa na Steven-Charles Jaffe
Bruce Joel Rubin
Howard W. Koch
Lisa Weinstein
Lauren Ray
Imetungwa na Bruce Joel Rubin
Nyota Patrick Swayze
Demi Moore
Whoopi Goldberg
Tony Goldwyn
Rick Aviles
Vincent Schiavelli
Muziki na Maurice Jarre (score)
Alex North
Imehaririwa na Walter Murch
Imesambazwa na Paramount Pictures
Imetolewa tar. Julai 13, 1990 (1990-07-13)
Ina muda wa dk. D.k. 128
Nchi Marekani
Lugha Kiingereza
Bajeti ya filamu Milioni $21
Mapato yote ya filamu $505,702,588

Hadithi hariri

 
Demi Moore na Patrick Swayze, katika moja ya kipande mashuhuri sana kutoka katika filamu hii[1]

Sam Wheat (Patrick Swayze), mkurugenzi wa benki, na Molly Jensen (Demi Moore) ni wapendanao wanaoishi mjini New York City.

Sam amegundua tofauti katika moja ya akaunti za washirika wake. Akamshauri rafiki na mtu mwenziwe katika kazi Carl Bruner (Tony Goldwyn), ambaye alitoa msaada wa kuchunguza, lakini Sam akaamua kuchunguza yeye mwenyewe. Muda mfupi baadaye Sam na Molly wakavamiwa na Willy Lopez (Rick Aviles). Sam akaauawa, lakini akabaki Duniani akiwa kama mzuka.

Sam akaonana na Oda Mae Brown (Whoopi Goldberg), tapeli msanii anayesimama kama mtu wa kati baina ya wafu na walio hai. Sam akagundua kwamba yule Oda Mae anaweza kumsikia. Sam akagundua kwamba uvamizi juu yake ulipangwa. Oda Mae akajaribu kumshawishi Molly kwamba mzuka wa Sam una muonya Molly juu ya hatari liomuhusisha Willy, lakini Molly akakataa kusikiliza. Carl akashitukia mpango mzima na kumshawishi Molly kwamba Oda Mae ni mlaghai. Sam akagundua kwamba Carl ndiye aliyepanga mauaji yake. Carl alihusika kinamna moja au nyingine katika njama za kuiba mamilioni ya mapesa ambayo Sam aliyashtukia - hivyo upelelezi wa Sam ungeharibu kila kitu.

Wakati Carl anajaribu kumtongoza Molly, Sam mwenye jazba akakurupuka, kwa bahati mbaya akagusa picha mjengoni pale. Sam akaenda kuomba msaada kutoka kwa mzuka ulio-katika njia za chini za reli (Vincent Schiavelli) ili ajue namna ya kuinua vitu vizito kwa akili bila kushika. Sam akamshawishi Oda Mae kuzuia mpango wa Carl kwa kuigiza kama ndiye mmiliki wa akaunti ya uongo ya Carl na kutoa fedha zote zilizopo kwenye akaunti hiyo, halafu kaifunga akaunti yenyewe.

Molly akaenda kituo cha poli kutoa taarifa juu ya mauaji ya Sam, lakini wakamshawishi na kumweleza kwamba ni mbinu za kujiamini tu za Oda Mae, almaarufu kama mlaghai. Carl akajaribu kuingia katika akaunti ile ya benki lakini kaikuta imefungwa. Sam akafanya uwepo wake kwa Carl, ambaye punde alijua kama ni kweli inatokea. Akamtakia Sam kwamba iwapo fedha hazitorudishwa, basi atamwua Molly.

Sam akashika zake njia mpaka nyumbani kwa Oda Mae kwenye kumuonya juu ya hatari inayotakiwa kufanywa na Carl na Willy. Sam akamkamata Willy kule, kamkandamiza kisawasawa. Willy akakimbilia mtaani na kugongwa na gari na hatimaye kufa. Oda Mae na Sam wakarudi nyumbani kwa Molly, kumshawishi Molly kwamba Oda Mae anaeleza ukweli mtupu. Oda Mae akamruhusu Sam na Molly kuwa pamoja kwa mara ya mwisho. Carl akajiri akiwa na mijazba ya kuua - Molly na Oda Mae wakatoroka. Sam, kaishiwa nguvu baada ya kumuingia Oda Mae, amedhoofikia kiasi kwamba vigumu sana kulipiza kisasi.

Sam akarudisha nguvu zake na kuwasaidia Molly na Oda Mae, na kumshinda Carl. Safari yake imeisha, Sam akasema kwaheri yake kwa mara ya mwisho na kuondoka zake mbinguni.

Washiki hariri

Stephen Root na mama wa mwongozaji Charlotte Zucker ameonekana katika filamu, akiwa kama jinsi alivyoonekana Phil Leeds akiwa kama mzuka wa hospitali.

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya Nje hariri