Too Much (wimbo)

(Elekezwa kutoka Too Much (Darassa))

"Too Much" ni jina la wimbo uliotoka 15 Julai, 2016 wa msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania - Darassa. Wimbo umetayarishwa na Mr. T. Touch. Huu ndio wimbo ambao huhesabiwa kama ujio mwingine au wa kivingine wa Darassa tangu Kama Utanipenda na zile za nyuma kabla ya hii. Kuanzia hapa, Darassa alibadili muundo wa kutambaa na michano tofauti na awali. Tangu wimbo huu, Darassa ameamsha hisia za watu kila kona ya Tanzania. Hata baada ya kutoa Muziki alizidi kupendwa zaidi.[1]

“Too Much”
“Too Much” cover
Kava ya Too Much (wimbo)
Single ya Darassa
Imetolewa 15 Julai, 2016
Muundo Upakuzi wa mtandaoni
Imerekodiwa 2016
Aina Hip hop
Urefu 3:11
Studio Classic Music
Mtunzi Darassa
Mtayarishaji Mr. T. Touch
Mwenendo wa single za Darassa
"Kama Utanipenda"
(2016)
"Too Much (wimbo)"
(2016)
"Muziki"
2016

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri