Tropiki

eneo la Dunia linalozunguka Ikweta

Tropiki ni ukanda wa dunia uliopo pande zote mbili za ikweta kati ya latitudo za 23.5° za kaskazini na za kusini.

Kanda ya tropiki duniani

Ni ukanda wa joto duniani. Hapa jua linafikia mahali pa juu kabisa angani hivyo ukanda huu unapokea mwanga na joto zaidi. Katika maeneo kusini na kaskazini yake jua halifiki kamwe juu kabisa.

Pia hakuna tofauti kubwa katika muda wa mchana na usiku jinsi ilivyo nje ya tropiki kuelekea nchani. Hii ni pia sababu ya kwamba nchi za tropiki hazina majira kama maeneo yenye joto ya wastani au maeneo karibu na ncha za dunia.

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.