Tula (Siri ya Mtungi)
Tula ni jina la uhusika kutoka katika tamthilia ya Siri ya Mtungi kutoka nchini Tanzania. Uhusika umechezwa na Beatrice Taisamo. Tula ni mwanamke shupavu anayeitambua thamani yake. Mwenye uwezo wa kuhoji mambo kwa mapana. Ana mapenzi ya dhati kwa Cheche Mtungi, japo Cheche alimwacha. Kulingana na hadithi, Tula ndiye mwanamke wa kwanza wa Cheche, halkadhalika Cheche ndiye mwanaume wa kwanza wa Tula. Maisha na mikakati ikaja kuwatenganisha na Cheche kumuona Cheusi na Tula kubaki msela. Japo bado ana mapenzi ya dhati kwa Cheche. Tula ana biashara yake ndogo ya grosari.
Tula | |
---|---|
muhusika wa Siri ya Mtungi | |
Taswira ya Tula (Siri ya Mtungi) (uhusika umechezwa na Beatrice Taisamo) | |
Imebuniwa na | MFDI Tanzania |
Imechezwa na | Beatrice Taisamo |
Misimu | 1, 2 |
Maelezo | |
Jinsia | Kike |
Kazi yake | Mjasiriliamali |
Utaifa | Mtanzania |
Isitoshe, Cheche mawazo yake mengi huwa hajadiliani na mkewe, mara nyingi huja kwa Tula hasa kwa kufuatia Tula anamjua Cheche nje, ndani. Tula ana fikra pana sana katika maisha. Hababaiki, wala hasitushwi na lolote lile. Mwenye kupokea mawazo mapya kwa ajili ya mustakabali wa maisha yake. Baadaye alionekana kuungana na mtu mmoja aliyemwezesha kupanua biashara yake kwenye kiwango kile alichotaka. Cheche alipohoji muungano ule, alijibiwa si tu mwenza kibiashara, bali vilevile kuna mengine yanaendelea.
Alifanya jitihada nyingi kumrudisha Cheche mikononi mwake kikamilifu, shida tu Cheche na wanawe na mkewe, katu hawatenganishiki.[1]
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ Tula (Siri ya Mtungi) Archived 12 Septemba 2016 at the Wayback Machine. katika wavuti rasmi ya Siri ya Mtungi.