Tunguridi
Tunguridi | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Tunguridi ni ndege wadogo wa jenasi Pytilia katika familia Estrildidae ambao wanatokea Afrika tu. Wanafana na mishigi na wana rangi mbalimbali kama nyekundu, machungwa, njano na/au kijani. Hula mbegu hasa lakini wadudu pia, hususa makinda. Tago lao ni tufe la manyasi lenye mwingilio kwa kando. Jike huyataga mayai 3-4.
Spishi
hariri- Pytilia afra, Tunguridi Mabawa-machungwa (Orange-winged Pytilia)
- Pytilia hypogrammica, Tunguridi Mabawa-njano (Red-faced or Yellow-winged Pytilia)
- Pytilia lineata, Tunguridi Domo-jekundu (Red-billed Pytilia)
- Pytilia melba, Tunguridi Mabawa-kijani (Green-winged Pytilia au Melba Finch)
- Pytilia phoenicoptera, Tunguridi Mabawa-mekundu (Red-winged Pytilia)
Picha
hariri-
Tunguridi mabawa-njano