Twariqah Ahmadiyah Idrisiyah

Twariqah Ahmadiyah Idrisiyah (Twariqah dandrawiyah) ni miongoni mwa twariqa/njia za kisufi iliyoasisiwa na Sayyidina Sheikh Ahmad bin Idris mwanzoni mwa karne ya 19. Twariqa hii imeenea sana katika nchi za Uarabuni, lakini pia Afrika (Somalia na Tanzania), Indonesia, Malaysia, India na kwingineko duniani.

Historia

hariri

Twariqa hii iliasisiwa na Sayyidina Sheikh Ahmad bin Idris mnamo mwaka 1835. Baada ya kufa kwa sheikh Ahmad bin Idris ambaye alikua muasisi wa twariqa hii, ikaendelea kwa khalifah wake ambaye alikuwa ni Sayiduna Sheikh Ibrahim Al-rashid (Qadasallahu sirrahu). Shekhe Ibrahim Al-rashid aliiongoza twariqa hii mpaka alipofariki mnamo mwaka 1872.

Baada ya kufariki Sheikh Ibrahim Al-rashid twariqa hii aliongozwa na Sayiduna Sheikh Muhammad Al-dandarawi mpaka alipofariki mnamo mwaka 1907.

Twariqah hii ya Dandarawiyah inajulikana kwa urefu kama Al-twariqatul Ahmadi A-rashidiah Dandarawiyah ambalo ni mchanganyiko wa majina ya mwanzilishi wa Twariqah hii naye si mwingine bali Al-qutb Twariqah Al-rais Sayiduna Sheykh Ahmad bin Idris (Qadasallahu Sirrahu) na sheikh mwingine katika silsilah kabla yake Sayiduna Sheikh Muhammad Al-dandarawi (Qadasallah Sirrahu).

Waanzilishi wote hawa watatu walikuwa wakimuona macho kwa macho Mtume Muhammad na walikabidhiwa Twariqah kutoka mikononi mwa Mkuu wa darja Aleyhi swalat wa salaam.

Sheikh Muhammad bin Ahmad Al-dandarawi

hariri

Sheikh Muhammad Al-dandarawi (Qadasallahu Sirrahu) alizaliwa huko mji wa Dandara, nchini Misri mnamo mwaka 1813. Sheikh huyu alikuwa ni Muridi wa Sayidna Sheikh Ibrahim Ar-Rashid Qadasallahu Ruhahu, mbali ya kupewa khirqah ya Twariqah na sheikhe lake alirithi pia uchamungu, elimu na harakati za kida'awa kueneza twariqah hii katika miji mbali mbali duniani.

Yasemwa Murshid wa twariqah ni yeye mwenyewe Sayiduna Sheikh Muhammad (Qadasallahu sirrahu). Ingawa amefariki lakini kutokana na maneno yake mwenyewe ni kuwa yeye ni Murshid wa Twariqah wakati alipokuwa hai na hata akiwa amefariki. Njia hii inafanana na Twariqah Uwaysiyah (si Qadiri Uwaysia ya Afrika Mashariki) na hii ni kuwa mafungamano baina ya Muridi na Murshid wake yanaendelea kuwepo hata baada ya kufariki kwa Sheikh wa Twariqah.

Karama zake

hariri

Katika masimulizi ya karama zake, alikuwa na kijakazi na pia hicho kijakazi kama suria wake. Ikatokea kijakazi hicho kilifanya yasiosimulika na kijakazi huyo akamfuata Sheikh amuadhibu kwa kumpiga bakora. Sheikh alighadhibika akasema wewe kinakufaa kifo na si bakora. Basi Sheikh akavua Imama yake kisha akaanza kumuapiza yule kijakazi na papo hapo alianza kusikia maumivu makali shingoni kama akinyongwa na baada ya siku mbili yule kijakazi akawa amefariki.

Kuna kipindi watu walikusanyika wakawa wanataka kumjaribu kama Sheikh Dandarawi ana karama zozote na je yeye ni Murshid Kaamil, wakampanga mtu mmoja (aliyekuwa hai) na wakamvisha sanda kisha wakamuomba Sayiduna Sheikh kumswalia swala ya maiti. Sayiduna Sheikh akawaambia kwanza mtoeni huyu mtu, wakasisitiza amswalie, akawaambia tena mtoeni huyu mtu walipozidi kusisistiza akamswalia na amaaa walipomfunua yule mtu alikuwa amekwisha kufa kitaambo gani.

Ilitokea wakati wa swala mmoja katika maamuma alikuwa amekuja kuswali nyuma ya Sheikh katika swala ya jamaa alikuwa amebeba nyama aliyoifungiliza kwa utaalam ili isigundulike alichokibeba. Alipomaliza kuswali akawa amekwenda nyumbani na ukawashwa moto ili nyama ile ipikwe, ile nyama ilipikwa bila dalili yoyote ya kuathiriwa na moto hadi kuni zikiisha. Ikapita shauri waende kumweleza kadhia ile Sayiduna Sheikh Dandarawi, walipofika akawaambia huyu bwana aliswali nyuma yangu na ilihali akiwa amebeba nyama na hivyo ni athari ya kitu kuwa nyuma yangu hakishiki moto.

Sayiduna Sheikh alikuwa na wanawe Abul Abbas, na mdogo akiitwa Abdulwahab. Inasimuliwa kabla ya kifo chake sheikh alikuwa safarini kuelekea Syria kumtembelea binti yake. Binti yake akamuuliza baba ni nani utamuachia Twariqah?. Hapo bintiye alikuwa hajawahi kumuona nduguye Abul Abbas, Sheikh akamjibu nitamuachia Twariqah Abul Abbas na akija Shaam utamjua bila kuambiwa na mtu. Na kweli baada ya kufariki kwake huko mji wa Madinah mwanawe alishika Twariqah na alikwenda Syria. Alipofika dada mtu akamuona moja kwa moja akajua yule ndiye kaka yake na akafurahi kwa ukelele mkubwa wa furaha na kumuita kwa jina nduguye.

Kifo chake

hariri

Sayiduna Sheikh Muhammad bin Ahmad ad-Dandarawi Radhiallahu 'anhu alifariki katika mji wa Madinah, tarehe 29 Muharram 1909 AD (1327 AH).

Ijaza ya kuingia kwenye twariqa

hariri

Ilikuwa desturi ya twariqah kabla hujaingia na kuchukua twariqah(kunyweshwa Ijazah) ili lazima ukariri neno Laa ilaha ila llahu wallahu akbar mara 4. Nyuradi zao kubwa ni tatu, ambayo ni kukariri kwa wingi utajo (Tahlil), kukithirisha kumswalia Mtume Muhammad sana, na kukithiri kuleta Istighfar Kabir.

Marejeo

hariri

Faraidhul Maatharal Marwiyah' kilichoandikwa na Sayiduna Sheikh Ahmad bin Muhammad Said (Qadasallah) 1935.