Tyra Banks
Tyra Lynne Banks (alizaliwa 4 Desemba 1973) ni mwigizaji, mwanamitindo, mfanyabiashara na mwimbaji nchini Marekani.[1][2][3] Alipata umaarufu kama mwanamitindo alipokuwa kwenye miji ya Paris, Milan, London, Tokyo na New York. Banks ni mbunifu na mtangazaji mkuu wa kipindi cha America's Next Top Model. Yeye pia ni mbunifu wa True Buauty na mtangazaji wa kipindi cha mahojiano cha The Tyra Banks Show.
Tyra Banks | |
---|---|
Tyra Banks | |
Amezaliwa | Tyra Lynne Banks 4 Desemba 1973 Marekani |
Kazi yake | ni mwigizaji, mwanamitindo, mfanyabiashara na mwimbaji nchini Marekani |
Maisha yake
haririTyra Banks alizaliwa mjini Inglewood, California; mwana wa Carolyn na Donald Banks.[4] Wazazi wake waliachana pindi Tyra alipokuwa na miaka sita. Baadaye, Carolyn aliolewa na Clifford Johnson. Banks alisoma katika shule ya John Burroughs iliyopo mjini Los Angeles na kisha akaenda katika shule ya upili ya Immaculate Heart.
Kazi yake
haririMwanamitindo
haririTyra alianza uanamitindo alipokuwa darasa la 11.[5] Baadaye, alienda mjini Paris kwa ajili ya kufanya kazi hii. Katika wiki yake ya kwanza mjini Paris, Tyra alipata umaarufu na mafanikio yaliyovunja rekodi kwani ilikuwa mwanzo wake katika uanamitindo. Yeye alishirikiana Anna Sui, CoverGirl, Badgley Mischka, Bill Blass, Chanel, Christian Dior, Dolce & Gabbana, H&M, McDonald's, Pepsi, Nike, Victoria's Secret na Yves Saint Laurent. Yeye ameonekana kwenye majalada maarufu kama Vogue, Harper's Bazaar, Cosmopolitan na Elle. Mnamo 1997, Tyra alipokea tuzo la VH1 Award for Supermodel of the Year. Mwaka huo huo, yeye alikuwa Mwamerika mweusi wa kwanza kutokea kwenye kasha ya jalada la Victoria's Secret.[6]
Filamu na televisheni
haririBanks alianza kuigiza kwenye msimu wa nne wa kipindi cha The Fresh Prince of Bel-Air ambapo aliigiza kama Jackie Ames. Aliigiza kwenye vipindi kama Felicity, MADtv na The Price Is Right
Hivi sasa yeye ana kipindi cha mahojiano cha The Tyra Banks Show, kilichoanza mnamo 12 Septemba 2005. Vilevile, yeye ni hakimu kwenye kipindi cha America's Next Top Model. Mnamo 2008, Banks alishinda tuzo la Daytime Emmy Award kwa kazi yake kwenye The Tyra Banks Show.
Banks amesema kuwa ataigiza kama Ursula Nyquist kwenye kipindi cha Gossip Girl msimu wa tatu.
Muziki
haririBanks ameonekana kwenye video za muziki kama "Black or White" ya Michael Jackson, "Love Thing" ya Tina Turner na kwenye wimbo wa "Too Funky" ya George Michael.
Filamu
haririFilm | |||
---|---|---|---|
Mwaka | Filamu | Aliigiza kama | Maelezo |
1995 | Higher Learning | Deja | |
1999 | Love Stinks | Holly Garnett | |
2000 | Love & Basketball | Kyra Kessler | |
Life-Size | Eve Doll | ||
Coyote Ugly | Zoë | ||
2002 | Halloween: Resurrection | Nora Winston | |
Eight Crazy Nights | Victoria's Secret Gown | Sauti yake pekee | |
2007 | Mr. Woodcock | Mwenyewe | |
2008 | Tropic Thunder | Mwenyewe | |
2009 | Hannah Montana | mwenyewe | [7] |
Vipindi | |||
Mwaka | Kipindi | Aliigiza kama | Maelezo |
1993 | The Fresh Prince of Bel-Air | Jackie Ames |
Aliigiza kwenye vipindi vifuatavyo:
|
1999 | Felicity | Jane Scott |
Aliigiza kwenye vipindi vifuatavyo:
|
Just Shoot Me! | Mwenyewe |
Aliigiza kwenye vipindi vifuatavyo:
| |
2000 | MADtv | Katisha Latisha Parisha Farisha Johnson |
|
2003-hadi leo | America's Next Top Model | Hakimu | Tyra ni hakimu na mtunzi wa kipindi hiki |
2004 | American Dreams | Carolyn Gill | |
All of Us | Roni | ||
2005-2010 | The Tyra Banks Show | Mtangazaji | Kipindi cha mahojiano |
2009 | Gossip Girl | Ursula Nyquist |
Marejeo
hariri- ↑ Jason Clark (2008). "Tyra Banks:Biography on MSN". MSN. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-09-02. Iliwekwa mnamo 2008-07-18.
{{cite web}}
: Unknown parameter|=
ignored (help) - ↑ "ABC News: Tyra Banks Experiences Obesity Through Fat Suit".
- ↑ "Tyra Banks On It - Forbes.com". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-12. Iliwekwa mnamo 2010-01-29.
- ↑ "Tyra Banks Biography". FilmReference.com.
- ↑ Hirschberg, Lynn (1 Juni 2008). "Banksable". New York Times.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-09. Iliwekwa mnamo 2012-07-09.
- ↑ "'Hannah Montana' Film Scenes Shot In Cool Springs Mall". NewsChannel 5.com. 2008-05-28. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-29. Iliwekwa mnamo 2010-01-29.
Viungo vya nje
hariri- Tyra Banks at the Internet Movie Database
- Tyra Banks katika All Movie Guide
- banks Tyra Banks katika People.com
- The Tyra Banks Show website
- The New York Times profile/interview