"U.N.I.T.Y" ni jina la kutaja wimbo ulioshinda Tuzo za Grammy - ambao umeimbwa na rapa/mwigizaji Queen Latifah kutoka katika albamu yake ya mwaka wa 1993, Black Reign. Kibao kilitolewa mnamo tarehe 6 Januari, 1994, anakemea masuala ya utovu wa nidhamu dhidi ya wanawake, anagusia masuala ya kero za mtaani, unyanyasaji majumbani, na kutoa la moyoni juu ya wanawake wanavyochukuliwa katika tamaduni ya hip-hop.

“U.N.I.T.Y.”
“U.N.I.T.Y.” cover
Single ya Queen Latifah
kutoka katika albamu ya Black Reign
Imetolewa November 9, 1993 (US) January 6, 1994 (UK)
Muundo 12", CD single, cassette single
Imerekodiwa 1993
Aina Jazz rap
Studio Motown Records
Mtunzi Queen Latifah, Kier "Kay Gee" Gist wa Naughty By Nature
Mtayarishaji Kay Gee
Mwenendo wa single za Queen Latifah
"Just Another Day..."
(1993)
"U.N.I.T.Y."
(1993)
"Black Hand Side"
(1994)

Kutokana na ujumbe uliobeba, vituo vya redio na TV walipiga wimbo huu bila kujali maneno yake makali ambayo ni "bitch" (mbwa jike) na "hoes" (changudoa, mwuza mwili wake kwa kipato), ambayo yanatokea kila wakati katika mashairi yake, hasa katika kiitikio mstari unasema "who you callin' a bitch?!" ambayo unamalizia ubeti. Wimbo umechukua sampuli ya "Message from the Inner City" wa The Crusaders. Wimbo pia ulipata kuonekana kwenye ucheshi wa Living Single, mfululizo wa Latifah uliorushwa mwaka huohuo.

Kuna toleo jingine ambalo nalo lilipata kupigwa sana maredioni na kwenye ma-TV linaitwa "U.N.I.T.Y. (Queen Ruff Neck Boot)", ambalo lina mapigo sawa na toleo la kwenye albamu, limepunguza sampuli ya jazz na kuingizwa mikito ya kihip-hop zaidi. Vilevile inaweza kupatikana kama toleo safi kwenye "20th Century Masters: The Millennium Collection: The Best of Queen Latifah" & "Hip-Hop: Gold".

Mwaka wa 1995 wimbo ulishinda Grammy Award kwa ajili Best Rap Solo Performance. Wimbo umebaki kuwa wimbo pekee wa Latifah kutamba vilivyo nchini Marekani hadi leo hii, na wimbo wake pekee kufikia nafasi ya 30 kwenye chati za Billboard Hot 100.

Muziki wa video

hariri

Muziki wa video uliongozwa na Mark Gerard ambaye pia aliongoza wimbo wake wa "Just Another Day...". Katika video, Latifah anaendesha pikipiki, ambayo ilitengenezwa kwa ajili ya kaka yake Lance, ambaye alikufa katika ajali ya pikipiki mnamo mwaka wa 1992. Funguo anazozidaka mwanzoni na kuzivaa katika wimbo mzima ni funguo zake za pikipiki ya kaka yake.

Waliouza sura katika video ni pamoja na kundi la rap la Naughty by Nature.

Michakaliko katika chati

hariri

Wimbo ulipata mafanikio kwa kushika nafasi ya 23 kwenye chati za The Billboard Hot 100. Wimbo ulikuwa miongoni mwa single zilizotamba mno kwenye chati za Billboard Hot Rap Singles, kwa kushika nafasi ya #2; meshika nafasi ya #7 kwenye chati za Billboard Hot R&B/Hip-Hop Songs chart.

Nafasi ilizoshika

hariri
Chati (1994) Nafasi
iliyoshika
UK Singles Chart 74
U.S. Billboard Hot 100 23
U.S. Billboard Hot R&B/Hip-Hop Songs 7
U.S. Billboard Hot Rap Tracks 2

Chati za mwishoni mwa mwaka

hariri
Chati za mwisho wa mwaka (1994) Nafasi
U.S. Billboard Hot 100[1] 82

Toleo la remix, linalojulikana kama "Big Titty Remix", linapatikana katika single yake ya "Just Another Day...".

Katika vyombo vingine

hariri

Wimbo ulipigwa mwishoni mwa filamu ya mwaka wa 1996 Girls Town.

Marejeo

hariri
  1. "Billboard Top 100 – 1994". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-03-01. Iliwekwa mnamo 2010-08-27.

Viungo vya Nje

hariri