Uandishi wa insha ni utunzi wa mfuatano wa tungo zenye mtiririko unaoelezea kuhusu mada fulani. Pengine unaagizwa shuleni ili kumzoesha mwanafunzi kujieleza kwa maandishi.

Insha ya mwanasiasa Mjerumani Theodor Heuss alipokuwa shuleni, 1898.

Aina za insha

hariri

Kuna aina mbili za insha, nazo ni:

  • 1. Insha za kisanaa.
  • 2. Insha zisizo za kisanaa.

Muundo wa insha

hariri

Kimuundo insha imegawanyika katika sehemu kuu nne:

  • kichwa cha insha
  • utangulizi wa insha
  • kiini cha insha/lengo la insha
  • mwisho wa insha/hitimisho

Huandikwa mwanzoni kabisa mwa insha na pia kichwa cha insha huandikwa katikati kwa herufi kubwa na kupigiwa mstari. Mara nyingi kichwa cha insha huandikwa kwa maneno machache.

hariri

Utangulizi wa insha

hariri

Sehemu hii hufuata baada ya kichwa cha insha na pia hueleza kwa ufupi juu ya jambo linalojulikana.

Kiini cha insha/lengo

hariri

Hii ni sehemu kuu kabisa: sehemu hii hufuata baada ya utangulizi. Pia hii ndiyo sehemu ambayo mwandishi huelezea kwa undani zaidi kuhusu jambo analoliandika; kila jambo analolizungumzia katika sehemu hii lazima liwe katika aya. Kila hoja ya mada uliyopewa inatakiwa kukaa na kuelezewa kwenye aya yake yenyewe.

Mwisho wa insha/hitimisho

hariri

Ni sehemu ya mwisho ya insha: mwandishi hutumia msisitizo majumuisho ya ufupisho wa yote aliyoyaandika. Pia mwisho wa insha huanza katika aya.

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uandishi wa insha kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.