Insha
Insha ni kifungu cha maneno kilichopangwa kwa mpangilio maalumu wenye kueleza kuhusu jambo fulani uliopangwa katika aya.
Insha huwa inaelezea jambo fulani, kwa mfano: matukio ya mauaji, ugonjwa fulani, mmea fulani, mnyama na kadhalika.
Sehemu za insha
haririKwa kawaida insha ina sehemu kuu nne ambazo ni,
- Kichwa cha habari.
- Utangulizi wa insha.
- Kiini cha insha.
- Mwisho wa insha.
Kichwa cha habari
haririHii ni sehemu ya kwanza ya insha ambayo huandikwa kitu kinachotaka kuzungumzwa kwenye insha hiyo. Sehemu hii huandikwa kwa herufi kubwa na kupigiwa mstari mfano, MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA.
Utangulizi wa insha
haririHii ni sehemu ya pili ya insha ambapo mwandishi hueleza kwa ufupi kile ambacho angependa kwenda kukiongelea kwenye insha yake. Katika sehemu hii mwandishi huandika kwa ufupi tu kile anachotaka kukielezea.
Kiini cha insha
haririHii ni sehemu ya tatu katika insha. Sehemu hii mwandishi huelezea kwa undani zaidi kile kitu ambacho alipanga kukiongelea kwenye utangulizi na kwenye kichwa cha habari yake. Katika sehemu hii mwandishi hupanga mawazo yake katika aya, Kila wazo huwa na aya yake.
Mwisho wa insha
haririSehemu hii mwandishi huandika hitimisho la insha yake. Kwa kawaida sehemu hii huwa ni fupi na hupangwa katika aya nyingine.
Insha za vyuo vikuu
haririWanafunzi wa vyuo vikuu pia huhitajika kuandika mitungo ya insha ambayo ni tofauti na ya wale walio kwa shule za misingi na sekondari. Kwa walio shule za sekondari, wao hutoa mitungo yao kwa akili, yaani hubuni. Katika vyuo vikuu, mambo hubadilika ambako wafaa kunukuu vipengee vya vitabu tofauti na mitungo ya wengine ili uandike insha yako.
Kwa kawaida, insha hizi huitwa essays kwa lugha ya Kiingereza. Pia zinafuata kanuni fulani kama inavyoelezwa hapa.
Tazama pia
haririMakala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Insha kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |