Ubongo Learning

(Elekezwa kutoka Ubungo Learning)

Ubongo Learning ni kampuni iliyopo katika mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania inayohusika na kutengeneza vipindi vya elimu vya kwenye runinga kwa njia ya sanaa na filamu za watoto.

Ubongo Learning inatayarisha vipindi viwili vya kwenye runinga ambavyo ni Ubongo Kids kwa ajili ya watoto wa umri wa kati ya miaka saba hadi kumi na mbili, pamoja na kipindi cha Akili and Me kwa ajili ya watoto wa umri wa miaka 3 hadi 6,Katika kipindi cha miaka mitano Vipindi vya Ubongo vimekuwa maarufu zaidi katika bara la Afrika vikionyeshwa katika nchi tisa bikiwa na jumla ya watazamaji milioni moja.

Ubongo wamekuwa wakitengeneza majukwaa mbalimbali ya kuwakutanisha watoto katika bara la Afrika kupitia michezo ya kielimu kwa watoto wa rika mbalimbali pamoja na kuhamasisha uwepo wa tabia njema kwa watoto, kuwapa ulinzi na elimu [1]

Marejeo

hariri
  1. Borzekowski, Dina L.G. (Januari 2017). "A quasi-experiment examining the impact of educational cartoons on Tanzanian children". Journal of Applied Developmental Psychology (54): 53–59. doi:10.1016/j.appdev.2017.11.007. Iliwekwa mnamo Julai 9, 2019.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ubongo Learning kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.