Mkoa wa Dar es Salaam
Mkoa wa Dar es Salaam ni mojawapo ya mikoa ya Tanzania ulioko katika pwani ya mashariki mwa Tanzania. Unapakana na Mkoa wa Pwani upande wa magharibi, kaskazini, na kusini, huku upande wa mashariki ukipakana na Bahari ya Hindi. Ni mkoa mdogo zaidi kwa ukubwa wa eneo (km² 1,393 pamoja na visiwa vidogo 8), lakini una idadi kubwa zaidi ya wakazi nchini, ukiwa na watu takriban 5,383,728 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022,[1] tena ni kati ya majiji yanayokua haraka zaidi duniani. Ingawa Dodoma ni mji mkuu wa kisiasa, Dar es Salaam inabaki kuwa makao makuu ya taasisi nyingi za serikali, mashirika ya kimataifa, na sekta binafsi. Pia ni kitovu cha shughuli za biashara, uchumi, na usafirishaji nchini, na inahudumia pia nchi za jirani kupitia bandari ya Dar es Salaam.Mkoa huu una wilaya tano: Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo, na Kigamboni.







Wakazi asili wa eneo la mkoa ni Wazaramo ingawa kwa sasa kutokana na kukua na kupanuka kwa jiji, kuna makabila yote ya Tanzania, mbali ya wageni wengi kutoka nchi mbalimbali.
Majimbo ya bunge
haririWakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2020 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Ilala : mbunge ni Mussa Azzan Zungu (CCM)
- Kawe : mbunge ni Joseph Gwajima (CCM)
- Kibamba : mbunge ni (CCM)
- Kigamboni : mbunge ni Faustine Ndugulile (CCM)
- Kinondoni : mbunge ni Abbas Tarimba (CCM)
- Mbagala : mbunge ni Issa Ally Mangungu (CCM)
- Segerea : mbunge ni Bonna Mosse Kaluwa (CCM)
- Temeke : mbunge ni Abdallah Mtolea (CCM)
- Ubungo : mbunge ni Kitila Mkumbo (CCM)
- Ukonga : mbunge ni Jerry Silaa (CCM)
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
hariri- Sensa ya 2002
- (Kiingereza)Usalama katika Daressalaam Ilihifadhiwa 23 Septemba 2006 kwenye Wayback Machine.
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Dar es Salaam bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Dar es Salaam kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |