Ubuyu ni ungaunga wa rangi ya maziwa wa matunda ya mbuyu ukiwa na mbegu zake au bila mbegu.

Tunda la mbuyu nje na ndani.

Ubuyu umekuwa ni mmea wenye faida nyingi kwa mwili wa binadamu.

Faida za ubuyu

hariri

1. Unga wa ubuyu una vitamini C

2. Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kalshiamu (Calcium).

3. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini

4. Ina virutubisho vya kulinda mwili

5. Ubuyu una vitamini B3 na vitamini B2 ambayo ni mhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng’enyaji wa madini ya chuma,

6. Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C

7. Huongeza nuru ya macho

8. Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika

9. Ina magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno

10. Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo.

Hasa kwa wale waliovunjika mifupa wanahimizwa sana kutumia juice ya unga wa ubuyu kila siku ili kuendana na mahitaji ya mwili


  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ubuyu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.