Uhuru Park ni eneo la burudani karibu na eneo la kati la biashara la Nairobi, Kenya. Lina ziwa bandia na jumba la mikutano ambalo hutumika kwa mikutano ya kisiasa na ya kidini.

Uhuru Park, Mjini Nairobi
Nyayo Monument

Ina sifa mbaya kama eneo ambapo maandamano dhidi ya unyakuaji haramu wa ardhi ulivunjwa na serikali Moi kwa kutumia fujo nyingi.

Mwaka 1989, Wangari Maathai na wengi wa wafuasi wake walifanya maandamano katika hifadhi hilo, na kujaribu kusitisha ujenzi wa jumba la ghorofa 60 la 'Kenya Times Media Trust'. Alilazimishwa na serikali aache ofisi yake na alikuwa akishutumiwa bungeni, lakini maandamano yake na mwitikio wa serikali uliwafanya wawekezaji wa kigeni kufuta mradi.[1]

Mnamo Agosti 1996, kundi la Wakatoliki wakiongozwa na Askofu mkuu Kardinali Maurice Michael Otunga lilichoma rundo la kondomu katika Uhuru Park ili kupinga matumizi ya kifaa hicho kama njia salama ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.

Marejeo

hariri
  1. The Ecologist (2001). The Good, ya Bad, na Ugly. Ilipakuliwa 2008/04/13.

Viungo vya nje

hariri