Ulafi (pamoja na ulevi) ni hamu isiyoratibiwa ya kula (na kunywa).

Sehemu inayohusu ulafi katika mchoro wa Hieronymus Bosch kuhusu vilema vikuu saba na vikomo vinne vya binadamu.
Vilema vikuu

Tabia hiyo ina madhara makubwa kwa afya ya binadamu.

Inakadiriwa kuwa siku hizi mtu 1 kati ya 3 anakula kuliko mwili wake unavyohitaji, na hivyo anasababisha maradhi mbalimbali yampate.

Upande wa maadili unahesabiwa kuwa kimojawapo kati ya vilema vikuu, ambavyo ni mizizi ya dhambi nyingine.