Hieronymus Bosch, (aliyezaliwa Jeroen Anthonissen van Aken[1], takriban 1450 - 9 Agosti 1516) alikuwa mchoraji wa Uholanzi. Aliishi maisha yake yote mjini ’s-Hertogenbosch, Uholanzi, ambayo wakati ule ulikuwa mji mkuu wa Utemi wa Brabant, eneo ambalo lilijumuisha sehemu kubwa za Ubelgiji na Uholanzi ya kisasa.

Hieronymus Bosch

Taswira zake nyingi zinaonyesha majaribu, dhambi na adhabu katika kuzimu[2]. Picha mata nyingi hufanana na ndoto zisizolingana na uhalisia. Zililenga kuonya watazamaji kuhusu hatari za dhambi na adhabu zinazoweza kufuata kwenye kuzimu.

Leo kuna picha 25 pekee zinazojulikana kuwa naye bila shaka; Filipo II wa Hispania alikusanya idadi ya hizo, na sasa zinapatikana katika Jumba la Makumbusho la Prado, Madrid .

Picha hariri

 
Sehemu ya Bustani ya Furaha za Kidunia

Marejeo hariri

  1. Dijck (2000): pp. 43–44. His birth is undocumented. However, the Dutch historian G.C.M. van Dijck points out that the vast majority of contemporary archival entries state his name as being Jheronimus van Aken. Variants on his name are Jeronimus van Aken (Dijck (2000): pp. 173, 186), Jheronimus anthonissen van aken (Marijnissen ([1987]): p. 12), Jeronimus Van aeken (Marijnissen ([1987]): p. 13), Joen (Dijck (2000): pp. 170–171, 174–177), and Jeroen (Dijck (2000): pp. 170, 174).
  2. Catherine B. Scallen, The Art of the Northern Renaissance (Chantilly: The Teaching Company, 2007) Lecture 26