Ulindwanoni
Ulindwanoni ni kijiji cha kata ya Ufukutwa (msimbo wa posta 45719) kwenye Wilaya ya Kaliua (Mkoa wa Tabora). Kipo kilometa 5 magharibi ya Kaliua mjini. Kina wakazi wapatao 4,126 kwa sensa ya mwaka 2012.
Ndicho kijiji alichozaliwa mbunge wa Urambo Magharibi Juma Kapuya.
Wakazi wa eneo hili ni jamii za wakulima na wafugaji. Zao kuu la biashara linalolimwa ni tumbaku.
Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ulindwanoni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |