Umakanika wa anga
Umakanika wa anga ni tawi la elimuanga unaohusiana na miendo ya violwa vya angani. Kihistoria umakanika wa anga umetumia kanuni za fizikia (umakanika kawaida) kwa violwa kama nyota na sayari ili kuleta data kuhusu mahali pake.
Historia
haririUmakanika wa anga wa kisasa unlianzishwa na Principia ya Isaac Newton mnamo mwaka 1687. Jina katika kiingereza “celestial mechanics” ni jipya kuliko hivyo. Pierre-Simon Laplace alileta istilahi hii zaidi ya karne baada ya Newton.