Metaboli

(Elekezwa kutoka Umetaboli)

Metaboli (gir. μεταβολή metabolē, "badiliko"; pia: umetaboli[1]) inamaanisha jumla la michakato ya kikemia mwilini mwa viumbehai. Viumbehai vinahitaji nguvu, yaani nishati kwa kukua, kudumisha maisha yao na kufanya kazi. Nguvu hii inapatikana kwa njia ya chakula pamoja na pumzi. Ndani ya mwili mfumo wa mmeng'enyo wa chakula (tumbo, utumbo) inavunja chakula kwa vipashio vyake vya kikemia ambavyo vinatumiwa na mwili kama lishe. Vivyo hivyo oksijeni inayofika kwa njia ya pumzi inapitishwa mwilini kwa njia ya damu hasa. Kutokana na mmenyuko wa hivi vyote mwili unapata nishati ya kujidumisha na pia maada ya kujenga seli au sehemu nyingine za mwili. Vipashio visivyotumiwa tena vinaondolewa mwilini.

Umetaboli wote hutofautishwa katika hali mbili

  • Kataboli inayovunja maada ogania (kwa mfano chakula) kwa vipashio vyake vya kikemia na kuvuna nishati
  • Anaboli inayotumia nishati hii kwa kujenga molekuli kama proteini au Amino asidi.

Vimeng'enya (ing. enzymes) huwa na nafasi muhimu sana katika michakato hii maana vinatawala na kulenga mimenyuko ya kikemia mwilini.

Mfumo wa umateboli wa kiumbehai unaamua dutu gani ni za faida yaani lishe ni zisizo hasara yaani sumu. Kwa mfano kuna bakteria kadhaa zinazotumia sulfidi ya hidrojeni kama lishe ilhali ni sumu kwa wanyama. [2]

Kemikali za kimsingi

hariri

Kuna hasa aina tatu za molekuli zinazojenga miili ya wanyama, mimea na bakteria: amino asidi, kabohidrati na mafuta. Molekuli hizi ni za kimsingi kwa uhai. Kwa hiyo ama zinatengenezwa katika metaboli kwa kujenga seli na tishu ya mwili ama zinavunjwa katika mtaboli kwa kuzitumia na chanzo cha nishati kwenye mmeng'enyo wa chakula. Vipashio vya kemikali hizi zatumiwa katika metaboli kujenga DNA au protini.


Marejeo

hariri
  1. "Metaboli ni pendekezo la KAST, "umetaboli" la KKK/ESD, KKS haina pendekezo.
  2. Friedrich C (1998). "Physiology and genetics of sulfur-oxidizing bacteria". Adv Microb Physiol. Advances in Microbial Physiology 39: 235–89.