Umwagiliaji wa matone

Umwagiliaji wa matone ni mfumo wa kisasa kwa umwagiliaji wa mimea na hasa mazao. Maji hupelekwa polepole kwa mabomba au mipira yenye matundu madogo moja kwa moja hadi mguu wa kila mmea, karibu na mizizi yake. Mfumo huu unapunguza sana matumizi ya maji na pia shida nyingine mbalimbali.[1]

Mfumo wa umwagiliaji wa matone kwa tuta la mboga majani kwa ajili njia fupi ya maji
Bomba la umwagilishaji matone
Mfumo wa umwagiliaji matone shambani unaotumia mitambo
Nozeli ya kutoneshaji maji

Historia

hariri

Vyanzo vya mfumo huu vinajulikana kutoka China ya Kale ambako wakulima walizika sufuria za kauri katika ardhi karibu na miti na kuizijaza maji, Maji yalipita kwenye kuta za vyombo na kuingia udongo karibu na mizizi polepole. Wajerumani walitumia mabomba ya udongo wa ufinyanzi uliochumwa ndani ya ardhi kwa umwagiliaji kuanzia karne ya 19. Baada vita kuu ya pili ya dunia mtu wa Australia alianza kutumia mabomba ya plastiki yenye matundu.

Ilionekana ya kwamba mbinu huu ni rahisi lakini una hasara kama mpira ni ndefu. Matundu karibu na chanzo cha maji hutoa maji zaidi kuliko matundu ya mbali. Pia kama shinikizo katika mpira ni juu kidogo maji hayatokei kwa umbo la matone mbali kwa nguvu mno kama mwendo mfululizo. Mfumo huu uliboreshwa nchini Israeli na Simcha Bass aliyeongeza nozeli za kutonesha maji (ing. dripper au emitter). [2]

Katika maeneo ya joto kubwa mfumo wote hupelekwa chini ya uso wa ardhi kwa kupunguza tena upotevu kutokana na usimbishaji wa maji hewani.


Faida za umwagiliaji wa matone

hariri

Faida za umwagiliaji wa matone ni kama zifuatazo:

  • Matumizi ya maji ni kidogo
  • Mbolea wa chumvi unaweza kuongezwa katika maji na kufikishwa karibu na mizizi pekee, hivyo matumizi yake yapungua pia
  • Maji yapelekwa pale amboka mimea inayahitaji, siyo pale ambako haihitajiki
  • Magugu yanapungua kwa sababu hayamwagiliwi (isipokuwa sehemu iliyo karibu sana na mazao)
  • Hatari ya magonjwa wa fungus inapungua kwa sababu majani yanabaki makavu
  • mfumo unahitaji shinikizo kidogo tu na hii inapunguza gharama za nishati (diseli, umeme) kwa ajili ya pampu
  • hata pampu ni ndogo hivyo rahisi zaidi
  • Mmomonyoko wa ardhi shambani unapungua sana
  • Hatari ya kuongezeka kwa chumvi ardhini inapungua sana

Matatizo ya umwagiliaji matone

hariri

Hasara zinazoweza kutokea wakati wa kutumia umwagiliaji wa matone:

  • Gharama: mwanzoni gharama zinaweza kuwa juu kuliko umwagiliaji wa kawaida.
  • Kuoza: Mipira na vipande vya plastiki vinaweza kuoza kutokana na jua
  • Kuziba: kama filta, mipira, mabomba na nozeli jaziangaliwi ipasavyo sehemu za mfumo zinaweza kuzibwa na uchafu mdogomdogo
  • Magonjwa kadhaa: madawa kadhaa yanayopulizwa kwa juu yanahitaji maji kutoka juu , maji kwenye mizizi hayatoshi
  • Ufundi: Mfumo mdogo unaweza kutengenezwa na kila mtu mwenye uwezo kiasi. Lakini mifumo kwa shamba zima inahitaji ufundi unaoelewa tabia ya eneo, mitelemko, hali ya maji yanayopatikana
  • Usimamizi: mfumo unahitaji kuangaliwa mara kwa mara na mfanyakazi anayeuelewa. Mtu asiyejali anaweza kusababisha hasara kubwa. Kama bomba inavuja mfululizo matumizi ya maji huwa juu sana.
  • Wanyama wagugunaji: Panya na wengine wanaweza kuharibu mipira na mabomba ya plastiki wakitafuta maji

Marejeo

hariri
  1. Majadiliano katika bunge la Tanzania kuhusu usambazaji wa mfumo wa umwagiliaji wa matone
  2. http://www.irrigationtutorials.com/drip-emitter.htm Archived 21 Aprili 2014 at the Wayback Machine. Aina za nozeli za kutonesha maji zinaelezwa hapa