United Biscuits (kifupi:"UB") ni kampuni ya kimataifa ya kutengeneza vyakula kama biskuti za BN, biskuti za McVitie's, KP Nuts, Hula Hoops, Kaukau za Real McCoy's, vyakula vya Phineas Fogg, Jacob's Cream Crackers na Twiglets.

Logo ya Kampuni United Biscuits.

Kampuni hii iliorodheshwa katika Soko la Hisa la London na ilikuwa mojawapo ya kampuni katika orodha ya FTSE 100 lakini mwezi Desemba 2006 ilinunuliwa na kundi la Blackstone na Washirka wa PAI.

Historia hariri

United Biscuits ilianzishwa mwaka wa 1948 kutoka kuungana kwa McVitie & Price na Macfarlane Lang.

Mnamo mwaka wa 1972, ilinunua Carr's wa Carlisle ,waliotayarisha biskuti maarufu za Table Water.

 
Mojawapo ya bidhaa za United Biscuits

Kampuni hii ilimiliki Kampuni ya Wimpy(Mikahawa) kati ya miaka ya 1977 na 1989. Pia ilinunua kampuni ya vyakula baridi ya Ross Young (1988).

Kampuni ilinunuliwa Mei 2000 na Finalrealm, kikundi cha wawekezaji fedha, wakiwa pamoja na Nabisco Holdings Corporation: kama mpango wa biashara Ub ilipewa sehemu ya biashara ya Uropa ya Nabisco.

Kampuni iliuza Young's Bluecrest hapo mwaka wa 2001, ili ienedeshe sekta yake ya biskuti tamu vizuri zaidi.

Mnamo Septemba 2004, kampuni ilinunua sehemu ya Uingereza ya Kundi la Jacob la Biskuti la Groupe Dannone kwa bei ya £ 240 milioni.

Julai 2006,UB iliuza biashara yake ya Kusini mwa Uropa kwa wanunuzi Kraft Foods, ambayo iliacha mmiliki wake na kuanza kujitegemea.

Mnamo Oktoba 2006, Kampuni hii iliuuzwa kwa kundi la Blackstone na Washirika wa PAI. Mpango huo ulikamilika Desemba 2006.

Operesheni za UB hariri

Msingi wa biashara hii umo nchini Uingereza,ambapo hupika biskuti na vitafunio vingine chini ya majina mbalimbali yakiwemo: McVitie's na Twiglets.

Kampuni hii ina viwanda vingi katika nchi kadhaa kote Uropa kama vile Uholanzi, Ufaransa na Ubelgiji.

Makao makuu hariri

Makao makuu ya kampuni yako Hayes, Middlesex. Kituo kikuu cha usambazaji nchini Uingereza ni kile cha Ashby-de-la-Zouch,hapo pia kuna kiwanda cha kutayarisha vitafunio vya KP.

Mfumo wa UB hariri

'Mtandao wa UB' ulikuwa mtandao wa redio ya kutumikia viwanda vya Uingereza lakini ulifungwa 1979.Ingawaje,mtandao huu ndio ulioanzisha kazi ya mtangazaji maarufu wa redio wa Uingereza Steve Allen na wa televisheni Dale Winton

Tarehe 2 Novemba 2007 [1] ilitangaza kuwa biskuti zake za Crawford's Bourbon Cream zirudishwe. Sababu ikiwa, kulikuwa na uwezekano wa vipande vidogo vya chuma kuwa ndani ya biskuti.

Angalia pia hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu United Biscuits kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.