McVitie's
McVitie's ni jina la biashara ya chakula inayomilikiwa na United Biscuits.
Jina hilo linapata asili kutoka kampuni ya biskuti ya Scotland, McVitie & Price Ltd, iliyoanzishwa katika mwaka wa 1830 Rose Street mjini Edinburgh, Scotland. Kampuni hii ilihamia maeneo mbalimbali ya jiji kabla ya kukamilisha,katika mwaka wa 1888, kiwanda cha kuunda biskuti cha St Andrews katika Robertson Avenue katika Wilaya ya Gorgie.
Historia
haririIngawa kiwanda cha McVitie & Price kiliungua mwaka wa 1894, kilijengwa upya mwaka huohuo kikaendelea kufanya kazi hadi 1969, wakati kazi ilisimamishwa na kuhamishiwa Uingereza. McVitie & Price waliendelea na upanuzi na kuunda kiwanda kipya katika Harlesden(1910) na mjini Manchester (1917). Kampuni ilinunua jumba la uokaji la Edinburgh la Simon Henderson & Wana wake katika mwaka wa 1922. McVitie & Price ilijiunga na jumba jingine la uokaji la Scotland ,MacFarlane,Lang & Co.,mwaka wa 1948 ili kuwa Kundi la United Biscuits.
Bidhaa za McVitie's zinaundwa katika viwanda vitano vya Uingereza: viwanda viwili vya kitambo McVitie's vya Harlesden na Manchester, kiwanda cha kitambo cha MacFarlane,Lang & Co,kiwanda cha kuunda biskuti cha Victoria huko Glasgow,kiwanda cha kitambo cha Carr cha kutayarisha biskuti cha 1831Carlisle na kiwanda cha keki cha McVitie's(kiliitwa cha Riley's Toffee Works} huko Halifax.
Biskuti maarufu ya kwanza ya McVitie & Price ilikuwa McVitie's Digestive,biskuti ya aina hiyo ya kwanza kabisa,iliyoundwa na mfanyikazi mpya Alexander Grant. Biskuti hii ilipewa jina hilo kwa sababu kulifikiriwa kuwa soda ya kuoka ilikuwa inasaidia katika mfumo wa mwili wa kusaga chakula tumboni.
McVitie's Chocolate Homewheat Digestive iliundwa kwa mara ya kwanza katika mwaka wa 1925. Zaidi ya pakiti milioni 71 ya McVitie's Chocolate Homewheat Digestive hununuliwa Uingereza kila mwaka,yaani biskuti 52 kulwa kila sekunde. HobNobs iliundwa katika mwaka wa 1985 na aina nyingine kama hiyo ya chokleti ikaundwa mwaka wa 1987.
Katika mwaka wa 1947, McVitie & Price ilioka keki ya harusi ya Malkia Elizabeth na Luteni Philip Mountbatten.
Baadhi ya bidhaa za McVitie's ziliitwa McV mnamo mwaka wa 2002, lakini hii ilibadilishwa 2005 na toleo jipya la nembo ya McVitie's. Mwaka wa 2007, United Biscuits iliipa leseni ya McVitie's kwa Meiji Seika Kaisha Ltd ili waweze kupika biskuti hizo Ujapani.
Bidhaa zao
haririBiskuti
hariri- Digestives
- Ginger Nuts
- Hob Nobs
- Rich Tea
- Penguin Bar
- Gold Bar
Keki
hariri- Keki ya Golden Syrup
- Keki ya Jaffa
- Keki ya Tangawizi ya Jamaica
- Keki ya Lemon
Picha
haririTazama pia
haririMarejeo
hariri1. The National Archives of Scotland, McVitie & Price, Ltd, Ilihifadhiwa 27 Aprili 2020 kwenye Wayback Machine., 2007-11-02
2. United Biscuits, Historia yetu Ilihifadhiwa 27 Aprili 2020 kwenye Wayback Machine.,2007-11-06
3."Maeneo". United Biscuits. Ilihifadhiwa 24 Juni 2007 kwenye Wayback Machine.. 2007-08-16.
4. "McVitie's". United Biscuits. Ilihifadhiwa 9 Agosti 2007 kwenye Wayback Machine.. 2007-08-16.
5. "McVities Digestives ya Ujapani". nicecupofteaandasitdown.com. Retrieved 2007-08-16.
Viungo vya nje
hariri- United Biscuits - ukurasa wa McVitie's Ilihifadhiwa 26 Desemba 2013 kwenye Wayback Machine.