Wimpy ni jina la mikahawa ya kupika vyakula vya haraka (kama vibanzi) mijini; mikahawa hiyo ina makao makuu nchini Uingereza. Inajulikana sana kwa baga (aina ya chakula inayohusu nyama,mboga na jibini ama mkusanyiko tofauti katikati ya vipande) yao inayojulikana kama the Bender, ambayo hasa ni soseji ya frankfurter bali si baga.

Wimpy
Makao MakuuUfalme wa Muungano Uingerza

Hapo awali mikahawa hii ilijulikana kama Wimpy Bars na watu wengi bado huijua kwa jina hilo, licha ya jina hilo kuachwa miaka mingi iliyopita na jina "Wimpy" kutumika. Wamiliki wa sasa wa Wimpy huendesha kazi zao katika nchi kadhaa chini ya jina Wimpy International.

Historia

hariri

Wimpy ilijenga jina katika miaka ya 1950. Jina hili lilitokana na tabia ya J. Wellington Wimpy kutoka Popeye katuni iliyoundwa na E. C. Segar. Eddie Gold alikuwa akiendesha mikahawa 12 katika miakaya mapema ya 1950s ndipo akapata wazo la mikahawa ya kupika vyakula vya kupikwa haraka(mfano:vibanzi,kaukau na baga) iliwafikia wakurugenzi wa J. Lyons and Co. Lyons wakasajilisha jina hilo kwa matumizi nchini Uingereza na mwaka wa 1954 "Wimpy Bar" ya kwanza ilianzishwa katika Nyumba ya Lyons Corner, Coventry Street,London. Hapo mwanzoni, mikahawa hii ilikuwa sehemu ndogo ya mikahawa ya kawaida ya Corner House lakini ufanisi wa sehemu hizo ilifanya mikahawa tofauti ya Wimpy kuanzishwa ikiandaa vyakula vya aina ya baga pekee yake. Ilipofika miaka ya 1970,biashara ilikuwa imepanuliwa hadi ikawa na mikahawa elfu katika nchi 23.

 
Mkahawa wa Wimpy wa Windhoek, Namibia

Katika mwaka wa 1977, biashara hiyo ilinunuliwa na kampuni ya United Biscuits. Hapo miaka ya 1980s,Wimpy ilikuwa imeanza kupoteza soko lao kwa McDonald's, iliyokuwa imefungua mkahawa yao ya kwanza Uingereza katika mwaka wa 1974 na usimamizi mpya ilianza kunyoosha mienendo yao ya kibiashara kwa kubadilisha njia za jadi za kuandaalia watu chakula mezani. Katika mwaka wa 1989, biashara ya Wimpy iluzwa kwa Grand Metropolitan(sasa Diageo). Grand Metropolitan ilkuwa imenunua Burger King mwaka uliokuwa umepita na wakaanza kubadili mikahawa hiyo kuwa mikahawa ya Burger King. Hapo mnamo mwaka wa 1990,mikahawa iliyobaki 220 ya "huduma kwa meza" ilinunuliwa na usimamizi mpya ya 3i. Usimamizi mpya ulifanyika tena mwaka wa 2002.

Ingawa Wimpy ina idadi iliyopungua ya mikahawa nchini Uingereza, bado hupatikana katika baadhi ya miji na jiji,palipo na huduma za Roadchef na katika pahali za Dundee Megabowl. Matawi katika maeneo ya Roadchef na Megabowl kawaida huwa na huduma kwa kaunta kinyume na mpangilio wa huduma kwa meza. Pia kuna Wimpy katika Dunmail Park Shopping Centre Workington, Cumbria,wanapohudumia sinema iliyokuwa hapo na wanunuzi.

Mnamo tarehe 27 Februari 2007, Famous Brands, ambayo inamiliki mikahawa ya Wimpy katika Afrika ya Kusini, ilitangaza kwamba ilikuwa imenunua Wimpy Uingereza.Baada ya kuinunua kampuni ilibadilisha jina ili iwe sambamba na Wimpy Afrika Kusini.

Alama "mpya" inayotumika sasa ni ile iliyotumika na Wimpy Uingereza hapo miaka ya 1960s hadi 1980s.

Hivi sasa, Wimpy inabadilisha na kubadilisha mikahawa yake, operesheni iliyoanza tarehe 22 Oktoba 2007 na uzinduzi wa mpangilio mpya katika Benfleet,Essex. Katika Wimpy mpya kuna mapambo mapya , viti vya aina tofauti na kutumika kwa rangi ya asili ya Wimpy ya nyekundu na nyeupe. Ili kusaidia mpangilio mpya,kuna menu mpya pia na kampeni ya dhati inayofanywa.

Kimataifa

hariri

Matawi ya Afrika Kusini

hariri

Wimpy ilifunguliwa katika Afrika Kusini mjini Durban , 1967. Biashara hiyo iliuzw Bakers SA Ltd katika mwishoni mwa miaka ya 1970 na baadaye kununuliwa na Steers Holdings Group

Nchi nyingine

hariri

1976, Wimpy ilifungua mkahawa wao wa kwanza mjini Bogota, Kolombia. Pia kuna matawi ya biashara kama Wimpy Ujerumani ambako yaliyatangulia yale ya Marekani, Kuwait, Kupro, Saudi Arabia,Kenya na Beirut, Lebanon, India, Nepal,} na Bangladesh. Sasa inamilikiwa na Famous Brands ambayo hivi karibuni ilikamilisha ununuzi wa Wimpy Uingereza.

 
Mkahawa wa Wimpy, Huddersfield

Matawi ya Misri na Moroko

hariri

Wimpy ilikuwa na matawi mengi Misri na Moroko, ilikuwa mikahawa ya kwanza ya baga nchini Misri na ya pili nchini Moroko lakini ilifunga biashara yake yote katika nchi hizo mnamo 1998.

Wimpy ilikuwa na matawi katika New Zealand kama Hamilton na Nelson lakini sasa imefungwa isipokuwa moja ya Rotorua.

Matawi ya Ireland

hariri

Kuna matawi machache nchini Ireland, mengi yakiwa katika vituo vya petroli. Kuna mkahawa Urlingford,County Kilkenny(ambapo mabasi husimama yakienda Dublin ama Cork na moja Celbridge,County Kildare. Mengi yako katika stesheni za mafuta ya petroli za Petrogas(Applegreen), kama wanaomiliki Wimpy mingi huko. [5]

Matawi ya Kuwait

hariri

Wimpy ilifunguliwa jijini Al-duiya Kuwait katika miaka ya 1970s.

Matawi ya Marekani

hariri

Wimpy ilifunguliwa katika mwaka wa 1969 katika mji wa Dallas, Texas na inahudumia eneo la magharibi ya mji wa Dallas na Oak Cliff. Wimpy ilisherehekea miaka 40 ya huduma tarehe 24 Agosti 2009.

Mr Wimpy

hariri

Katika miaka ya 1980, matangazo kwa mikahawa ya Wimpy ilionyesha katuni aitwaye Mr Wimpy. Yeye alikuwa karibu kufichika chini ya kofia kubwa, na pua na tabasamu tu ndiyo ilikuwa inayoonekana. Katika baadhi ya matawi, wafanyakazi walivaa sera ya Mr Wimpy kwa sherehe za watoto. Mr Wimpy pia alionekana katika mchezo wa kompyuta rasmi yaa Ocean software, iliyotolewa mwaka wa 1984 katika mifumo ya ZX Spectrum, Commodore 64 na mengineo.

Ingawa jina la awali lilitokana na tabia ya katuni ya Wimpy wa katuni ya Popeye,Mr Wimpy hakufanana na Wimpy wa Popeye.

Viungo vya nje

hariri