Upuge
Upuge ni kata ya Wilaya ya Uyui katika Mkoa wa Tabora, Tanzania, yenye msimbo wa posta namba 45215.
Jina la Upuge lilitokana na neno la lugha ya Kinyamwezi lenye maana ya mbwamwitu. Hapo zamani eneo hili kulikuwa na uwanja mkubwa kama eneo la bonde la maji walipokaa hao mbwamwitu. Kutokana na hilo, jina likaendelea mpaka sasa.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa 7,499 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 26,969 [2].
Makabila makubwa ya kata hiyo ni Wanyamwezi, Watutsi, Wasukuma, Waha na Wasumbwa.
Utamaduni ni kama jando na unyago, pamoja na ngoma ya asili maswezi.
Tanbihi
haririKata za Wilaya ya Uyui - Mkoa wa Tabora - Tanzania | ||
---|---|---|
Bukumbi | Goweko | Ibelamilundi | Ibiri | Igalula | Igulungu | Ikongolo | Ilolangulu | Isikizya | Isila | Kalola | Kigwa | Kizengi | Loya | Lutende | Mabama | Magiri | Makazi | Miswaki | Miyenze | Mmale | Ndono | Nsimbo | Nsololo | Nzubuka | Shitage | Tura | Ufuluma | Upuge | Usagari |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tabora bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Upuge kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |